Home LOCAL TUJITOKEZE TUSAJILIWE – WADAU HUDUMA YA MAJISAFI

TUJITOKEZE TUSAJILIWE – WADAU HUDUMA YA MAJISAFI

Watoa huduma ya magari ya majisafi katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wameendelea kusajiliwa na kuhamasisha wengine kujitokeza kwa wingi ili kisajiliwa.

Mmoja wa wamiliki wa magari ya usambazaji majisafi anayefanya shughuli hizo katika kituo cha kuchota majisafi eneo la Mbezi Spencon Bw. Linny Sangawe amewataka watoa wamiliki wengine kujitokeza ili kufanya kazi hiyo kwa halali.

Bw. Sangawe amesema huduma za usajili zinafanyika kwa wakati na kwa viwango kwa kizingatia maelekezo ya vigezo vilivyotolewa na DAWASA.

Aidha ameiomba Mamlaka isimamie maoni ya wadau ambayo wametoa ikiwa ni kudhibiti magari ambayo hayajasaliwa ili kuhajikisha ubora na viwango vya huduma.

“Kwa kweli usajili umetuongezea thamani ya huduma yetu kwa wateja wetu” alisema na kuongeza kuwa ni lazima sasa wenye magari hayi watoe ushirikiano kwa DAWASA ili kusajiliwa kabla ya Juni 30, 2023.

“Sisi tuliosajiliwa tutawapa ushirikiano DAWASA kwa kutoa taarifa ya magari ambayo bado hayajajisajili ili tudhibiti huduma, Alisema.

Alibainisha pia kuwa kuna baadhi ya wenye magari hayo husambaza maji ya yasiyo salama kutoka kutoka visima vya watu binafsi na baadaye kuharibu taswira ya huduma hiyo muhimu.

Naye Meneja wa Usimamizi wa Ankara DAWASA Bi. Asimwe Lukiko ameeleza kuwa DAWASA itaendelea kuzingatia maoni ya wadau waliyotoa katika kipindi cha usajili ambapo baada ya zoezi kukamilishwa hakuna gari ambalo halijasajiliwa litaruhusiwa kuchota maji katika vituo vya DAWASA.

“Tunashukuru watoa huduma ya usambazaji majisafi kwa magari kwa kujitokeza na kusajiliwa na kitutoa rai kwa wote kujitokeza kwani ni takwa la kisheria kupitia muongozo uliotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA” alisema Asimwe.

Alikumbusha pia kuwa usajili unafanyika kwa gharama ya Tsh 100,000 tu ambayo inalipwa kupitia malipo ya mfumo wa Serikali baada ya kupatiwa namba ya kumbukumbu.

Lengo la usajili huu ni kuratibu huduma ya majisafi zinazotolewa na sekta binafsi kupitia magari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here