Home LOCAL KINAMAMA WATANO WAFANYIWA UPASUAJI KUPITIA MATUNDU MADOGO

KINAMAMA WATANO WAFANYIWA UPASUAJI KUPITIA MATUNDU MADOGO

Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na wataalamu wa Alsalam Internatinal Hospital ya nchini Misri, imefanya kambi ya upasuaji wa kupitia matundu madogo (Laparoscopy surgery) kwa muda wa siku mbili ambapo kina mama watano wamenufaika na matibabu hayo.

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo leo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Upasuaji wa Matundu Madogo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Vincent Tarimo amesema waliofanyiwa upasuaji huo wengi walikuwa na changamoto ya uvimbe kwenye kizazi.

“Upasuaji wa matundu madogo hufanyika kwa kutoboa sehemu ndogo ya mwili kwa kuingiza vifaa maalumu ambapo una faida nyingi kwa kuwa mgonjwa hapati majeraha makubwa na uvujaji wa damu hivyo kupona haraka ili kuendelea na shughuli zake baada ya muda mfupi” amesema Dkt. Tarimo.

Previous articleWACHIMBAJI MADINI KUJIFUNZA KEKNOLOJIA MPYA CHINA
Next articleTUJITOKEZE TUSAJILIWE – WADAU HUDUMA YA MAJISAFI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here