Home SPORTS NHC KUSHIRIKI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI

NHC KUSHIRIKI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO NCHINI

Na: Eleuteri Mangi, WUSM, Dodoma
 

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Hamad Abdallah ambapo wamejadiliana namna kuendeleza ushirikiano baina ya pande mbili ili kuendeleza miundombinu ya michezo nchini.

Kikao hicho kimefanyika Juni 07, 2023 katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linatekeleza miradi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwemo jengo la ofisi za Wizara linalojengwa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma pamoja na eneo la changamani la michezo Kawe jijini Dar es Salaam.

Previous articleGGML YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUTOA ELIMU KUHUSU AINA ZA TAKA, UGAWAJI VIFAA
Next articleKAMATI YA USIMAMIZI WA MPANGO WA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA TANZANIA (MKUMBI) YAKUTANA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here