Home BUSINESS NCT YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI JIJINI DAR

NCT YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI JIJINI DAR

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uelewa mpana kwa wadau wanaotoa huduma katika Sekta nzima ya Utalii nchini, Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kimetoa mafunzo kwa watoa huduma za chakula na wafanyabiashara wa samaki katika soko la Kimataifa la Samaki Feri Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika leo Juni 1, 2023 katika soko hilo, Mkufunzi Mwandamizi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), na Matibu wa Mafunzo hayo Bi. Elina Makanja, amesema kuwa Chuo hicho kimekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo mbalimbali kwa wadau waliopo katika mnyororo wa thamani ili kiuwajengea uwezo na uelewa mpana katika utoaji wahuduma zao.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yamekuja kutokana na umuhimu wa soko hilo ambalo limekuwa likitembelewa na wageni wa mataifa mbalimbali ya kigeni.

“Chuo kimefanya mafunzo haya lengo kubwa likiwa ni kuboresha huduma katika sekta nzima ya utalii na huduma kwa watalii wanaokuja nchini, na pia kwa kufanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii na kuwapa huduma mbalimbali kama mchango wetu kwa ujumla.

“Tunafahamu kwamba Chuo kinafanya juhudi hizi za mafunzo kwa wadau mbalimbali mara kwa mara na kuwafanya kuwa na uelewa wa namna ya kuwahudumia wateja katika sekta nzima ya utalii.

“Kama ambavyo mnafahamu, kuna juhudi kubwa za Serikali yetu katika kuongeza watalii hapa nchini, ambapo Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni ‘Tour Guide’ namba moja amefanya jitihada kubwa kuhakikisha watalii wanaongezeka kupitia filamu maarufu ya ‘Tanzania the Royal Tour’ inayoendelea kufanya vizuri katika Mataifa mbalimbali Duniani” Ameeleza Bi. Makanja.

Kwa upande wake Mkufunzi aliyeongoza mafunzo hayo Bw. Jafari Mwemtsi  amesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na mwitikio mkubwa na kwamba, wamefikia lengo kutokana na idadi kubwa ya mahudhurio ya wadau waliojitokeza kwa wingi kwenye mafunzo hayo.

Naye Mwenyekiti wa Wavuvi wadogo wadogo Amiri Amani amesema kuwa mafunzo hayo yamewafumbua macho na kukiri kuwa kuna mambo mengi waliyokuwa wakifanya kinyume na utaratibu, hususani katika maadalizi ya chakula na bidhaa zake kwa ujumla, hivyo watatumia semina hiyo kuwaelimisha wengine.

Previous articleCHONGOLO ATAKA UPANUZI UWANJA WA NDEGE NDULI UKAMILIKE IFIKAPO AGOSTI 2023
Next articleCHONGOLO AHITIMISHA ZIARA YAKE IRINGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here