Home LOCAL CHONGOLO ATAKA UPANUZI UWANJA WA NDEGE NDULI UKAMILIKE IFIKAPO AGOSTI 2023

CHONGOLO ATAKA UPANUZI UWANJA WA NDEGE NDULI UKAMILIKE IFIKAPO AGOSTI 2023

Na: Mwandishi wetu, IRINGA.

Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amemtaka mkandarasi anayejenga Uwanja wa Ndege wa Nduli Mkoani Iringa ahakikishe kuwa unakamilika ifikapo Agosti mwaka huu, huku akitoa Rai kwa Wananchi Mkoani humo kuhakikisha wanautumia vizuri Uwanja huo, ili waweze kunufaika na fursa ya uwepo wake kwa Kujiimarisha Kiuchumi kupitia Sekta ya Kilimo na Utalii kwenye Ukanda huo.

Komredi Chongolo ametoa rai hiyo leo Juni Mosi, 2023, baada ya kukagua mradi wa upanuzi Uwanja wa Ndege Nduli, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku saba ya kukagua uhai wa CCM, Utekelezaji ilani ya uchaguzi ya Chama hicho ya 2020-2023 pamoja na Kuzungumza na Makundi mbalimbali ya Kijamii.

“Uamuzi wa Serikali kuujenga upya uwanja wa ndege wa Nduli, dhamira yake kubwa ni kuanza kufungua fursa kwa wananchi wa mikoa ya kusini kuweza kusafirisha bidhaa na Biashara mbalimbali zinazotokana na Sekta ya Kilimo.

Pia amesema Wananchi wa Kanda ya Kusini wanatarajia kunufaika kupitia Sekta ya Utalii baada ya Uwanja wa Ndege wa Nduli Kukamilika, ambapo fursa ya ujio wa Wageni kutembelea vivutio vya Utalii itakuwepo ambapo wananchi watapata fedha na Serikali itaongeza mapato.

Katika hatua nyingine katibu mkuu huyo wa CCM komredi Chongolo amewakumbusha Wakazi wa Iringa kuendelea kutunza utamaduni wa mkoa huo ili wageni wanaoingia wajue na Kujifunza tamaduni za mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Katibu Mkuu komredi Daniel Chongolo katika ziara yake hiyo ameambatana na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu.

Previous articleDKT. KIRUSWA ATOA ONYO KWA WAFANYABISHARA WA MADINI YA JASI
Next articleNCT YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA SOKO LA SAMAKI FERI JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here