Home LOCAL FIDIA YA ARDHI INA UMUHIMU ZAIDI KULIKO FIDIA YA FEDHA – CHONGOLO

FIDIA YA ARDHI INA UMUHIMU ZAIDI KULIKO FIDIA YA FEDHA – CHONGOLO

Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo amewataka wananchi wa Kata ya Ng’ambi Wilayani Mpwapwa kutokubali fidia ya fedha na badala yake wachukue fidia ya ardhi kwa maendeleo ya muda mrefu.

Chongolo ameyasema hayo alipotembelea mradi mkubwa wa bwawa la Msagali lililopo Kata ya N’gambi linalojengwa kwa zaidi Shilingi Bilioni 27.

Chongolo amesema kukamilika kwa bwawa hilo kutasaidia katika shughuli za kilimo cha umwagiliaji,ufugaji na binaadamu, hivyo wananchi wapewe fidia ya ardhi karibu na mradi huo ili wanufaike nao.

Katika hatua nyingine amewaasa wananchi kuacha kuuza maeneo yao yaliyo karibu na Mradi kwa manufaa yao ya sasa na baadae.

Amesema kuna baadhi ya watu ambao wamejitokeza kuwalaghai wananchi ili wawauzie maeneo yao, kwa kuwa wanajua Faida itakayopatikana.

Kutokana na hilo amewaagiza viongozi wa eneo hilo kudhibiti ulanguzi wa ardhi unaofanywa na baadhi ya watu kwa wanachi wa eneo hilo.

Mradi huo wa Bwawa la Msagali unaogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 27 linatarajiwa kujazwa maji lita Bilioni 93 ambazo zitasaidia katika shughuli za kiuchumi na Kijamii.

Previous articleRAIS DKT. SAMIA APOKEA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 45 KUTOKA BENKI YA NMB
Next articlePICHA: HAFLA YA MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA MAFANIKIO YA BENKI YA NMB
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here