Home BUSINESS COSTECH YAENDELEA KUTENGENEZA SERA KWA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILI KUONGEZA...

COSTECH YAENDELEA KUTENGENEZA SERA KWA MATUMIZI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA ILI KUONGEZA UFANISI KATIKA UZALISHAJI VIWANDANI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Profesa Lughano Kusiluka na mgeni rasmi katika Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu na  Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt.  Amos Nungu wakizindua kitabu kinachoelezea Mchango wa Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika Maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania kutoka katika Taasisi kumi za Utafiti na Maendeleo kwenye kilele Cha kongamano hilo.

(PICHA NA JOHN BUKUKU)

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Profesa Lughano Kusiluka na mgeni rasmi katika Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu akikabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya shilingi Bilioni moja Kwa Tiberius Mario mmoja wa wabunifu watakaonufaika na Fedha hizo za serikali Kutoka COSTECH ili kukuza wabunifu nchini kwenye wakati wa kilele Cha kongamano hilo Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt.  Amos Nungu

NA: NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeendelea kutengeneza sera kwa ajili ya matumizi ya Sayansi na Teknolojia ili kuwezesha sekta za uzalishaji nchin kuwa na matokeo yenye tija kwa Taifa.

Akizungumza leo tarehe 16/6/2023 Jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda wakati akifunga Kongamano Kitaifa la 8 la Sayansi na Teknolojia na Ubunifu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Profesa Lughano Kusiluka, amesema kuwa serikali inatambua kazi ambazo wanafanya wabunifu wa kisayansi na teknolojia na kuleta tija kwa Taifa.

Profesa Kusiluka amesema kuwa maendeleo yenye kasi hayawezi kufikiwa bila kuwa na jitihada, hivyo wameendelea kutafuta rasilimali ili kuhakikisha kila mtu anashiriki katika sayansi, teknolojia na ubunifu.

“Tume ya Sayansi na Teknolojia imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya utafiti, ubunifu kwa ajili ya kuhakikisha tuna kwenda sawa na utaratibu wa ulimwengu wa kufika katika maendeleo endelevu ambayo yanategemea sayansi Teknolojia” amesema Profesa Kusiluka.

Amesema kuwa katika Kongamano hilo limekuwa fursa kwa serikali katika kuonesha mipango yake kwani wote wanajua kuwa Sayansi na Teknolojia ni kichocheo kikubwa sana katika maendeleo ya jamii na ulimwenguni.

Amesema kuwa anawashukuru taasisi zote za utafiti ikiwemo vyuo vikuu kwa kuja kwa wingi kushiriki katika kongamano hilo.

“Nimefuraishwa na ushiriki wa wanafunzi wa shule ya msingi na Sekondari, ambao tunawategea kuwa watafiti, wabunifu na maprofesa wa miaka ijayo hivyo tunapoenda mambo yatakuwa mazuri” amesema Profesa Kusiluka.

Ameeleza kuwa katika Kongamano hilo maeneo mahususi matano yamejadiliwa na watafiti pamoja na wabunifu katika kuhakikisha malengo husika yanafikiwa.

Amebainisha kwa mada zilizojadiliwa pamoja na Mapinduzi ya nne ya viwanda, Sayansi, Teknolojia na ubunifu kwa uchumi wa kijani, uchumi ustamilivu na uchumi Jumuishi.

Mada nyengine ni ubunifu kwa maendeleo ya watu, mchango kwa maarifa asilia katika maendeleo ya sayansi na teknolojia na ubunifu pamoja sayansi huria na sera.

“Mada hizo zimebeba mambo mengi sana na yote yanalenga katika kuhakikisha Taifa letu linafikia malengo ya dira ya mwaka 2050 na tumebakiwa na miaka miwili kufikia lengo” amesema
Profesa Kusiluka.

Amesema kuwa wote wanafahamu lengo la dira ya maendeleo ni kuwaletea watanzania maisha bora, kuinua kiwango cha elimu, kudumisha utawala bora, utawala wa sheria, kujenga uchumi imara wenye uwezo wa kukabiliana na ushindani, kuimarisha amani, umoja na utulivu miongoni mwa watanzania.

Amesema kuwa ili kufikia malengo mchango wa wananyasi, watafiti, wabunifu wajasiliamali pamoja na wananchi inaitaji kwa maslahi mapana ya Taifa.

Profesa Kusiluka amesema kuwa Kongamano hilo ni sehemu ya kuboresha na kuendeleza, sera, kanuni, miundo ya sayansi na teknolojia katika nchi hasa katika kipindi hiki ambapo nchi imeanza maandalizi ya kuandaa mpango wa miaka mitano kuanzia mwaka 2025.

“Naamini mmekaa kwa siku tatu na kujadili mambo mbalimbali, mawazo yenu yatachukuliwa na kuchakatwa na kuwa sehemu ya dira, Costech wameandaa kongamano wakati muafaka” amesema Profesa Kusiluka.

Kongamano 8 la Kitaifa la Sayansi Teknolojia na Ubunifu limefanyika kwa siku tatu kuanza tarehe 14 – 16 /2023 ambapo kauli mbiu ni Sayansi na Teknolojia na ubunifu kwa maendeleo endelevu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here