Home BUSINESS COSTECH: KUENDELEZA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KWA MAENDELEO YA TAIFA

COSTECH: KUENDELEZA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA UBUNIFU KWA MAENDELEO YA TAIFA

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) COSTECH , Dkt. Amos Nungu , tarehe 20 Juni 2023 wakati akifanya mahojiano na kipindi maalumu cha twendepamoja cha Kituo cha Channel 10 kilichoangazia Mafanikio ya COSTECH katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita (6) inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan – Jijini Dar es salaam

Dkt Nungu alisema kuwa kupitia Sheria Na 7 ya Bunge la Tanzania ya Mwaka 1986, COSTECH ilianzishwa nchini Tanzania ili kukuza na kuendeleza Sayansi , Teknolojia na Ubunifu na kutambulika kama mrithi Baraza la Taifa la Utafiti Ilianzishwa mwaka 1972 ili kuongeza tija na Serikali ikaanzishq Tume ya Taifa inaendelea kuitumikia Tanzania hadi sasa.

Dkt. Amos Nungu ameongeza kuwa kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, COSTECH imefanya kazi kwa bidii kutafuta fedha kutoka vyanzo vya ndani na nje ya nchi. Kupitia Mfuko wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE), COSTECH imeweza kukusanya takriban TZS Bilioni 1 zitakazosaidia kuendeleza miradi ya utafiti na ubunifu. Wiki iliyopita, COSTECH pia ilifanikiwa kuandaa Kongamano la Kimataifa kupitia mkutano na maonesho wa STICE uliofanyika tarehe 14 – 16 Juni 2023, na kufanikiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na pamoja na washiriki zaidi ya 600 walishiriki kwa njia ya mtandao.

Dkt. Nungu amefafanua kuwa mojawapo ya jukumu muhimu la COSTECH ni kuratibu wataalamu kutoka taasisi za utafiti na maendeleo (R&D’s) pamoja na vyuo vikuu (HLI) . COSTECH inaratibu juhudi za utafiti na inahakikisha kuwa watafiti wanakuja na suluhisho la changamoto zinazokabili jamii.

” Mfano mzuri wa jitihada za COSTECH ni mradi wa kuongeza uzalishaji wa zao la mchikichi katika Mkoa wa Kigoma. Mradi huo ulipokea ufadhili wa Tsh Milioni 120 kutoka COSTECH, pamoja na mbunifu Magilatech, alibuni mfumo wa tigobackup unaomsaidia mtu kurudisha mawasiliano yake ikiwa alipoteza simu ” alisema dkt. Nungu

COSTECH pia inaendesha Kamati ya Tuzo za Sayansi na Teknolojia (TASTA) ili kukuza ubunifu na kusaidia wabunifu katika nyanja mbalimbali. Aidha, COSTECH baada ya kuonzisha muongozo wa Kitaifa wa mwaka 2008 imekuwa ikiaratibu mashindano ya MAKISATU kwa miaka mitatu (3) mfululizo toka 2019, 2020, 2021, 2022 na kwa mwkaa huu tumeazimisha Wiki ya ubunifu ili kutoa tathimini ya kuona bidhaa za kibunfu zinazoalishwa nchini na kuongeza mnyonyoro wa thamani kwa mfumo wa kibunifu Kitaifa

Aidha, kupitia Shindano la Kitaifa na maonesho ya MAKISATU, COSTECH imekuwa ikiwapata wabunifu wenye vipaji na kuwapa mafunzo na ruzuku. Hadi sasa, COSTECH imeweza kuwezesha vijana zaidi ya 2600 na kutoa ruzuku ya jumla ya Bilioni 1.79 kwa vijana 47 walioonyesha uwezo mkubwa katika ubunifu na walipewa hundi hiyo kupitia Konagamo la STICE lilifanyika kwa Siku tatu (3) kuanzia tarehe 14 – 16 Juni 2023 , Ukumbi wa JNICC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here