Home SPORTS YANGA SC YAHESABU MASAA MACHACHE KUTUA DIMBANI ‘SAUZ’

YANGA SC YAHESABU MASAA MACHACHE KUTUA DIMBANI ‘SAUZ’

KIKOSI Cha Yanga kimebakiza masaa machache kucheza mchezo wa marudio wa nusu fainali ya pili kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF Confederation Cup).

Kikosi hicho leo kitavaana na Marumo Gallants ya Afrika Kusiniki ikiwa ni mchezo wa marudiano hatua ya nusu fainali katika  Uwanja wa Royal Bafokeng Stadium, nchini huko .

Awali timu hizo zilikutana katika Dimba la Benjamini Mkapa, Jijini Dar es Salaam na Yanga ikiibuka kidedea kwa mabao 2-0.

Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Azizi Ki pamoja na Benard Morrison kipindi cha pili.

Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Nasredinne Nabi awali kabla ya kuelekea nchini humo alisema  anahitaji ushindi katika mchezo huo ili kuweza kucheza fainali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here