Home SPORTS YANGA SC YAHESABU MASAA MACHACHE KUTUA DIMBANI ‘SAUZ’

YANGA SC YAHESABU MASAA MACHACHE KUTUA DIMBANI ‘SAUZ’

KIKOSI Cha Yanga kimebakiza masaa machache kucheza mchezo wa marudio wa nusu fainali ya pili kwenye Mashindano ya Kimataifa ya Kombe la Shirikisho la Afrika (CAF Confederation Cup).

Kikosi hicho leo kitavaana na Marumo Gallants ya Afrika Kusiniki ikiwa ni mchezo wa marudiano hatua ya nusu fainali katika  Uwanja wa Royal Bafokeng Stadium, nchini huko .

Awali timu hizo zilikutana katika Dimba la Benjamini Mkapa, Jijini Dar es Salaam na Yanga ikiibuka kidedea kwa mabao 2-0.

Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Azizi Ki pamoja na Benard Morrison kipindi cha pili.

Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Nasredinne Nabi awali kabla ya kuelekea nchini humo alisema  anahitaji ushindi katika mchezo huo ili kuweza kucheza fainali.

Previous articleBENKI YA NBC YATOA GAWIO LA SHILINGI BILIONI 6 KWA SERIKALI
Next articleDART KUJENGA CHUO CHA MAFUNZO YA MADEREVA WA BRT, KITATOA MAFUNZO PIA KWA MADEREVA KUTOKA NJE YA NCHI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here