Home SPORTS WEMA KAIJINGI AWATAKA WALIMU KUWEKA RATIBA ZA MICHEZO SHULENI

WEMA KAIJINGI AWATAKA WALIMU KUWEKA RATIBA ZA MICHEZO SHULENI

Na: Heri Shaaban (Bagamoyo)

Afisa Elimu Msingi na Elimu awali Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ,Wema Kajigili amewataka Walimu Wakuu wa shule za Msingi na Waratibu Elimu Kata kutenga kila ijumaa siku ya michezo na kuandaa vitalu vya michezo mbalimbali Ili kupata wachezaji Bora .

Afisa Elimu Wema Kajigili alisema hayo wilayani Bagamoyo Viwanja vya Kalenge wakati wa ufunguzi mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya wilaya.

Alisema mashindano ya UMITASHUMTA kuunda timu ya Wilaya ufanyika kila mwaka katika halmashauri ya Bagamoyo ambayo huusisha shule zote za Msingi .

Akizungumzia mafanikio alisema wachezaji wamepata muda wa kutosha kuonesha vipaji vyao hasa mpira wa miguu wavulana Netiball ambapo ushirikiano baina ya Walimu wa michezo uliongezeka kwenye mashindano hayo.

Aidha alisema Walimu wa michezo walibadilishana uzoefu katika nyanja mbalimbali za sekta ya michezo na kujenga umoja na mahusiano.

Akizungumzia Kauli mbiu ya michezo ya UMITASHUMTA mwaka huu 2023 alisema Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo uimalishaji wa Miundombinu ya Elimu nchini ni chachu ya Maendeleo ya Taaluma Sanaa na Michezo”

Ameshauri mapendekezo Kamati ya Uratibu michezo Wilaya iandaae mpango mkakati wa kukagua vifaa vya michezo mashuleni pamoja na miundombinu .

Akizungumzia mashindano ya Umitashumta mwaka huu 2023 alisema wamepanga kupeleka Wanafunzi kwenye michezo mbali mbali Ikiwemo Sanaa za maonyesho na fani za Jukwaa ,mpira miguu ,mpira Netball,Riadha (miruko na mitupo)
Mpira wavu wavulana ,mpira mikono wavulana

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Majid Muhina, aliwataka Wanafunzi wasizarau michezo kwani michezo uwafanya Wanafunzi wafanye vizuri darasani hivyo Wanafunzi wasikate tamaa katika sekta michezo .

Kaimu Mkurugenzi Muhina alitaka apewe taarifa za shule na Wakuu wa shule ambao hawashiriki michezo mashuleni

Alisema sekta elimu Bagamoyo inafanya vizuri kila mwaka kitaaluma aliwataka wasimamie michezo ili waweze kukitangaza Halmashauri hiyo ya Wilaya .

Aliagiza Waratibu Elimu na Walimu Wakuu kuweka mpango kazi ,mkakati katika sekta michezo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here