(PICHA NA: EMMANUEL MBATILO)
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ndege ya Serikali kwaajili ya kuusafirisha mwili wa Mwanza habari marehemu William Malecela ambaye ni wa Mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu John Samuel Malecela.
Akizungumza Leo Mei 15, 2023 wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kumuaga mwili wa marehenu Lemutuz katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaaam, Meya wa Jiji la Dar es Salaam Matahiki Omar Kumbilamoto amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia imetoa ndege kuusafirisha mwili wa Lemutuz.
Amema Rais Samia ndege aina ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba wa 70 kuusafirisha mwili wa Lemutuz, nakwamba wamepongeza na kumshukuru kwa kitendo hicho cha utu alichoonyesha kwa watanzania.
“Tunamshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuonesha utu wake kwa Watanzania, tunamshukuru kwa kutoa usafiri kumsafirisha ndugu yetu Lemutuz.” Amesema Kumbilamoto.
Akimzungumzia Lemutuz amesema alikuwa ni mtetezi mkubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia alikuwa akiwatetea hata watu binafsi kwenye mitandao ya kijamii na hakika vijana wanapaswa kuendelea pale ambapo Lemutuz ameishia.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuikimbilia familia ya Waziri Mkuu mstaafu Malecela kwa kuamua kutoa usafiri wa ndege kuusafirisha mwili wa Lemutuz.
“Kuna rafiki yetu mmoja aliomba ushauri kwa William lakini akamwambia hawezi kumsadia na hataki kuwa mnafiki, hivyo unaweza kuona Lemutuz alikuwa anasimama kwenye ukweli na hakuwa mnafiki.” amesema Mhe. Silaa.
Naye kaka wa William Malecela, Samuel Malecela akizungumza alipokuwa akitoa wasifu wa marehemu, amesema William amezaliwa Machi 25, 1961/katika kijiji cha Mvumi mkoani Dodoma.
Alipata elimu yake ya msingi Mvumi na baadae alijiunga na Shule ya Sekondari ya Mazengo na alipomaliza elimu ya sekondari alienda nchini Marekani ambapo alipata Shahada mbili na kisha kuamua kuishi huko.
Marehemu Lemutuz ameacha watoto wawili wanaoishi Marekani.
Credit, Said M. Msagala