Home Uncategorized MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MIANZINI...

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MIANZINI – NGARAMTONI MKOANI ARUSHA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mianzini – Ngaramtoni Juu yenye urefu wa kilometa 18 leo tarehe 18 Mei 2023 akiwa ziarani mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango, Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela pamoja na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Rogatus Mativila.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikata utepe wakati wa ukaguzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara katika hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mianzini – Ngaramtoni Juu yenye urefu wa kilometa 18 leo tarehe 18 Mei 2023 akiwa ziarani mkoani Arusha. Wengine katika picha ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango, Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya, Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Rogatus Mativila, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Selemani Kakoso.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia viongozi pamoja na wananchi mbalimbali wa mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya Mianzini – Ngaramtoni Juu yenye urefu wa kilometa 18 leo tarehe 18 Mei 2023 akiwa ziarani mkoani Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Watanzania kutumia kwa usahihi barabara zinazojengwa kwa kuondokana na mwendokasi na kutozingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazojitokeza.

Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Barabara ya kiwango cha lami ya Mianzini – Ngaramtoni Juu yenye urefu wa kilometa 18 akiwa ziarani mkoani Arusha leo tarehe 18 Mei 2023. Amesema taifa linaendelea kupoteza nguvukazi kwa vifo na ulemavu wa kudumu kutokana na matukio ya ajali za barabarani.

Amewasihi madereva wa vyombo vya moto kuwa waangalifu,watumiaji wa bodaboda kuzingatia kofia ngumu pamoja na abiria kuvaa mikanda wawapo safarini. Pia amewahimiza Askari wa Usalama barabarani kusimamia sheria kikamilifu pasipo kuwaonea wananchi na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Halikadhalika Makamu wa Rais amemuagiza mkandarasi anayejenga barabara ya Mianzini – Ngaramtoni Juu kutoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wa mkoa wa Arusha ili waweze kunufaika na mradi huo muhimu.

Makamu wa Rais amesema serikali ya awamu ya sita imeonesha nia ya dhati na vitendo katika kuboresha miundombinu hususani maeneo ya vijijini ambapo tangu kuingia madarakani imeongeza bajeti ya TARURA kutoka bilioni 275 mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia bilioni 818.02 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 utakaoanza mwezi julai. Ameongeza kwamba lengo ni kuhakikisha barabara za vijijini zinapitika vema na kwa urahisi ili kuchochea shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya amesema ujenzi wa barabara hiyo unalenga kufungua upya miundombinu katika Wilaya ya Arumeru na kuwapa unafuu zaidi wananchi kuyafikia masoko katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kwa gharama nafuu na muda mfupi zaidi.

Pia amesema barabara hiyo itatumika kama barabara ya mchepuko (bypass) ili kupunguza msongamano katikati ya jiji la Arusha.

Ujenzi wa barabara ya Mianzini – Ngaramtoni Juu kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 18 inagharimu shilingi bilioni 22.2.

Previous articleUKWELI KUHUSU MGOMO WA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO
Next articleRAIS SAMIA AKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO, UWEKEZAJI VIWANDA NA BIASHARA,TRA PAMOJA NA KATIBU MKUU KIONGOZI IKULU DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here