Home BUSINESS KAFULILA: SERIKALI IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO MAREKEBISHO YA SHERIA YA UBIA

KAFULILA: SERIKALI IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO MAREKEBISHO YA SHERIA YA UBIA

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM

Serikali ipo katika hatua za mwisho za marekebisho ya Sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) ambapo hatua hizo zitawezesha utakelezaji wa miradi kuwa nzuri zaidi ikilinganishwa na huko nyuma.

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) David Kafulila,  wakati wa kikao kazi kati yake na Wahariri wa habari kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kilichofanyika leo Mei 16,2023 Jijini Dar s Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Idara hiyo kuhusu namna inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

Amesema kuwa majukumu hayo yamegawanywa na Serikali ambapo yapo baadhi majukumu yakafanywa na sekta binafsi na serikali yenyewe ikafanya baadhi ya majukumu ambayo sekta binafsi hayawezi kuyafanya.

“Jambo hili la PPP kwa nchini kwetu limeanza kutambuliwa tangu awamu ya nne kwa kiasi kikubwa kwa maana ya ya utekelezaji umeanza tangu awamu ya kwanza. tumekuwa na huduma Fulani Fulani ambayo Serikali ina ubia na sekta binafsi” 

Ameendelea kusema kuna sifa ambazo sekta binafsi inatakiwa kuwa nazo ikiwemo mkataba wa muda mrefu na viatarishi ambavyo inazibeba.

“Utekelezaji wa miradi ya PPP ulianza wakati wa Serikali ya awamu ya nne ambapo mwaka 2010 ilitungwa Sheria na kufuatiwa na kanuni zilizotungwa mwaka 2011, Sheria hii ilifanyiwa marekebisho mwaka 2014 na kufuatia marekebisho mengine ya Sheria hiyo yaliyofanyika mwaka 2018.

“Kwa Sasa marekebisho makubwa ya Sheria hiyo yapo kwenye hatua nzuri, na Sheria inakuja kumlinda mwekezaji tofauti na huko nyuma ambapo hakukuwa na Sheria nzuri kwa ajili ya kutekeleza miradi kwa njia ya ubia .

“Wakati wa utekelezaji wa miradi ya PPP miradi mingine itaibuliwa na kuletwa na sekta binafsi na mingine italetwa na Serikali na msingi wa PPP ni kuifanya sekta binafsi ifanye majukumu ambayo yangefanywa na Serikali,”amesema Kafulila.

Previous articleMAKAMU WA RAIS ATETA NA WANANCHI WA MONDULI MKOANI ARUSHA
Next articleCHALAMILA ATUA DAR KWA KISHINDO AIBUKIA SOKO LA MWENGE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here