Home LOCAL CHALAMILA ATUA DAR KWA KISHINDO AIBUKIA SOKO LA MWENGE

CHALAMILA ATUA DAR KWA KISHINDO AIBUKIA SOKO LA MWENGE

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amefanya ziara ya Kustukiza katika Soko la Mwenge ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo baada ya kuhamishwa kituo cha kazi na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoka Kagera.

RC Chalamila akizungumza Mara baada ya kufika katika Soko hilo Leo Mei 16, 2023 amesema dhamira ya kupita kwenye maduka mbalimbali ni Kujionea hali halisi ya kinachozungumzwa na Wafanyabiashara mitaani.

“Pamoja na kuwa Sijaingia Ofisini Rasmi lakini nimeona ipo haja ya Kusikia hasa huku mtaani watu wanasema nini, lakini katika moja eneo nililopita watu wanalalamikia uwepo wa Kodi kubwa zisizoweza kulipwa na Wafanyabiashara kutokana na Kiwango kikubwa cha VAT ambayo ni asilimia 18” amesema Chalamila.

Aidha RC Chalamila amesema Suala lingine ambalo linalalamikiwa na Wafanyabiashara hao ni kuhusiana na Idara ya Forodha ambayo imeweka viwango vikubwa vya Kodi hasa katika Vitenge pamoja na mlolongo mrefu wa Ufuatiliaji ambapo ni kikwazo kwa wafanyabiashara wengi.

“Jambo la Tatu ambalo nimelisikia ni kuwepo kwa zoezi la Kamata kamata kwa Wafanyabiashara Kariakoo na kuwakosesha Uhuru pamoja na Kuleta Usumbufu kwa Wateja wao na hasa kwa Wateja kutoka Kongo, Zambia, Malawi pamoja na mataifa mengine” ameeleza RC Chalamila.

Pia Mkuu huyo wa mkoa amesema kingine alichobaini kwa Wafanyabiashara katika eneo la Mwenge ni Kuwepo kwa Wafanyakazi Wanafunzi ambao wanatumiwa na Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) ambao wanakuwa hawana uwezo wa lugha nzuri na yenye staha kwa Wafanyabiashara.

“Jambo lingine ni Utaratibu wa TRA kuruhusu mizigo kutoka Bandarini na Baadae tena Wanakuja Kukagua nyaraka Sehemu za Kuhifadhia Mizigo (Godown), jambo ambalo wafanyabiashara wanasema ni Usumbufu mkubwa kwao”

“Kubwa zaidi ni Kauli ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya Kusamehe Kodi ya Miaka mitatu au Mitano nyuma, ambapo Wafanyabiashara hawajaweza kuichukua kauli ya Rais Kwa Vitendo, ambao Sasa TRA wamekuwa wakiomba Barua Rasmi kutoka kwenye Mamlaka hizo kwa Maana ya Rais, Waziri Mkuu au Makamu wa Rais” amebainisha RC Chalamila

Previous articleKAFULILA: SERIKALI IPO KATIKA HATUA ZA MWISHO MAREKEBISHO YA SHERIA YA UBIA
Next articleSERIKALI YASHAURI VYAMA VYA WAFANYAKAZI KUJIUNGA TUCTA ILI KULETA UFANISI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here