Home SPORTS YANGA SC YAMOTO, YAICHAPA RIVER UTD 2-0 KWAO

YANGA SC YAMOTO, YAICHAPA RIVER UTD 2-0 KWAO

Timu ya Wananchi Yanga SC imeichapa timu ya Rivers United ya Nigeria mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua Robo ya Fainali, mchezo huo umepigwa katika uwanja wa  Godswill Akpabio nchini Nigeria.

Magoli ya Yanga yalipachikwa Kambani katika Kipindi cha pili cha mchezo huo dakika ya 74 ya mchezo huo likifungwa na Fiston Mayele akiunganisha pasi safi ya nahodha Bakari Mwamnyeto.

Goli la pili lilipatikana katika dakika ya 81 ya mchezo huo likifungwa na Fiston Mayele akimalizia mpira uliopigwa na Bakari Mwamnyeto baada ya kupiga counter attack na kuwaacha mabeki wa Rivers.

Kwa matokeo hayo Yanga SC imejiweka katika mazingira mazuri ya kutinga hatua ya nusu Fainali ya mashindano hayo kutokana na idadi hiyo ya magoli.

Timu hizo zinatarajia kurudiana kati ya Aprili 29 au 30, mwaka huu katika Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Previous articleMTOTO ALIYESAIDIWA MATIBABU NA RAIS SAMIA ATOA SIMULIZI YA KUSISIMUA
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 24,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here