Home LOCAL WANAJESHI KAMBI YA KABOYA KAGERA WAKOSHWA NA WIZARA YA AFYA KUTOA ELIMU...

WANAJESHI KAMBI YA KABOYA KAGERA WAKOSHWA NA WIZARA YA AFYA KUTOA ELIMU KUHUSU UGONJWA WA MARBURG

Na. Elimu ya Afya kwa Umma .

Katika jitihada za Serikali za kuhakikisha kila jamii inafikiwa  na elimu kuhusu  tahadhari na kujikinga dhidi ya  ugonjwa wa Marburg baada ya kuripotiwa Mkoani Kagera,  Askari  wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ)  Kambi ya Kaboya Wilayani Muleba Mkoani Kagera wamevutiwa na  hatua zinazofanywa na Wizara ya Afya za uelimishaji kuhusu  tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

Akizungumza  mara baada ya kutembelea  kutoa elimu katika kambi ya Jeshi Kaboya Wilayani Muleba Mkoani Kagera, mwakilishi kutoka Wizara ya Afya,Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma  Beauty Mwambebule amesema Wizara ya Afya, na Wadau wengine wana wajibu wa kuhakikisha kuwa Taasisi zote zinafikiwa na elimu hii ikiwemo Majeshi,  ambapo katika kambi hiyo takriban wanajeshi 72 wameweza kupatiwa elimu ya ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Marburg.

“Pamekuwa na hamasa ya juu sana katika eneo hili la jeshi ambapo kikubwa ambacho nimekiona katika kambi la jeshi hili ni ule utayari wa kuomba na familia  zao ziweze kufikiwa na  elimu ya ugonjwa wa Marburg na sisi kama Wizara ya Afya na  Ofisi ya  Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera tupo tayari “ amesema.

Aidha, Beauty ameushukuru uongozi wa Kambi ya Jeshi Kaboya  kwa  kuahidi kuja na mkakati wa kuhakikisha kila mwanajeshi anakuwa na vitakasa mikono ,  kuweka maeneo ya kunawa mikono  ikiwa ni pamoja na katika ngazi ya familia ambapo pia Wizara ya Afya imetoa  ndoo za kunawia katika kambi hiyo.

“Mwitikio wa wanajeshi ni mzuri sana ,  kwanza wamehakikisha kila Mwanajeshi hapa ana vitakasa mikono ambacho  kinatia moyo kuwa Taasisi kama hizi wapo tayari kupambana na magonjwa ya mlipuko na kila  kstation point wapo tayari kuweka ndoo yenye maji tiririka na sabuni ya maji kwa ajili ya kunawa ili kukabiliana na ugonjwa huu “ amesema.

Awali Mkuu  wa Kambi ya Jeshi ya Kaboya  Kamanda Luten Kanali Saleh Nia ameishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea na hatua za uelimishaji kila Taasisi huku akiomba elimu ya ugonjwa wa Marburg itolewe pia katika familia za wanajeshi  ndani ya kambi hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi(JWTZ) katika kikosi  cha  Kaboya akiwemo 2Lt  Charles Kakuyu pamoja na  2Lt Irene Aaron Lukyaa  wamesema kupitia elimu waliyoipata itawasaidia kujikinga na ugonjwa wa Marburg .

“Kuanzia leo nimejifunza namna ugonjwa huu unavyoweza kuenezwa  kupitia wanyamapori ,majimaji mwilini  na dalili zake mfano kutokwa na damu, pia nimejifunza kuwa iwapo nitaona kuna mtu ana dalili nina wajibu wa kutoa taarifa mamlaka husika au kupiga simu bure           199” amesema 2Lt Irine Lukyaa”.

MWISHO

Previous articleSHIRIKINI KWENYE MIRADI ILI MUWEZE KUIMILIKI NA KUIVUTIA SERIKALI KUIENDELEZA” MBUNGE  MTATURU
Next articleNEEMA KIUSA AWATAKA WATANZANIA KUISHI KATIKA MATENDO MEMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here