Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali baada ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo, Dar es Salaam, Miongoni mwa wageni waaalikwa kwenye futari hiyo ni Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa.
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa akitoa salamu kwa wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania .Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam wakiongozwa
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa (katikati) waliokaa mbele akiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Fatma Abdallah ( wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energy Tanzania Dk Suleiman Majige ( wa pili kulia)
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energy Tanzania Dk . Suleiman Majige ( wa pili kulia) wakibadilishana mawazo na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa( kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
Na: Mwandishi Wetu
KAIMU Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa ameipongeza Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kuwaunganisha Watanzania kupitia programu zake mbalimbali za kibiashara.
Amesema kampuni hiyo inajali kazi zake, kwa sababu ni chombo cha kibiashara na moja ya utaratibu wa biashara ni kuvuta soko ambalo halipatikani bila kutanguliza mapenzi ya dhati ya shughuli zake.
Sheikh Walid alitoa pongezi hizo, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo, Dar es Salaamna kuhudhuriwa na wageni wadau mbalimbali akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Fatma Abdallah na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energy Tanzania Dk. Suleiman Majige.
Alisema walichokifa Puma Energy Tanzania, kimeonesha wameelewa maagizo ya Mwenyezi Mungu ya kutaka watu kuishi pamoja, huku akisisitiza kampuni hiyo inajali kazi zake.
“Niwapongeze Puma Energy Tanzania, kwa wakati huu tuliokuwepo wa Mwezi wa Ramadhan, ambao Mwenyezi Mungu anatuagiza tufanye mengi ya kheri yanayomridhisha yeye,” alisema.
Alisisitiza kwamba kampuni hiyo inajali kazi zake kwa sababu ni chombo cha kibiashara na moja ya utaratibu wa kibiashara ni kuvuta soko ambalo halipatikani bila kutanguliza mapenzi ya dhati kwa shughuli zake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania, Dk. Suleiman Majige, alisema wanaendelea kuiombea kampuni hiyo kwani ni mali ya Watanzania, iendelee kufanya kaza vizuri.
Pia, Dk. Majige iliishukuru Menejimenti ya Puma Enery Tanzania kwa kazi walioifanya ya kuwaunganisha na kuwakaribisha katika hafla hiyo, pamoja na kuwatakia mfungo mwema wa Ramadhani inayoendelea.
Aidha amewataka kuwa karibu na Mungu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni muhimu kumuomba Mungu kila wakati aendelee kuleta neema na mapenzi mema.
Mwisho