Home LOCAL NEEMA KIUSA AWATAKA WATANZANIA KUISHI KATIKA MATENDO MEMA

NEEMA KIUSA AWATAKA WATANZANIA KUISHI KATIKA MATENDO MEMA

Mkurugenzi wa Taasisi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akikabidhi Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa Certificate of Gratitude Katika madhimisho ya Siku matendo mema Duniani iliyoandaliwà na Fahati Tuamke Maendeleo (Picha na Heri Shaaban)

Mwenyekiti wa Umoja wanawake (UWT )Wilaya ya Ilala Neema Kiusa akimpatia Certificate Of Gratitude Balozi wa Mazingira Wilaya ya Ilala HERI SHAABAN kituo Cha Afya Chanika Aprili 14/2023 wakati wa uzinduzi wa kupanda miti Jimbo la Ukonga kituo Cha Afya Nguvu Kazi Chanika katika Madhimisho ya siku ya matendo Mema Duniani hafla iliyoandaliwà na Fahari Tuamke Maendeleo

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa akipanda miti na Mkurugenzi wa Fahari Tuamke MAENDELEO katika siku ya Matendo Mema Duniani kituo Cha Afya Nguvu Kazi Chanika (Picha na Heri Shaaban ) 

Viongozi wa Chama na Jumuiya wakiwa na Mwenyekiti wa Umoja wanawake UWT Wilaya ya Ilala Neema Kiusa Kata ya Chanika wakati wa kupanda miti kituo Cha Afya Nguvu Kazi Kata ya Chanika siku ya matendo Mema Duniani Aprili mwaka huu , hafla iliyoandaliwà na Taasisi ya Fahari Tuamke MAENDELEO (Picha na Heri Shaaban )

Na: Heri Shaaban (Ilala)

Mwenyekiti wa Umoja wanawake (UWT) Wilaya ya Ilala Neema Kiusa , amewataka Watanzania kuishi katika matendo mema ambayo yanampendezesha Mwenyezi Mungu tuache kuishi kwa kufuata utamaduni wa kuiga badala yake tuishi kwa kufuata Mira za kitanzania.

Mwenyekiti wa Umoja WANAWAKE WIlaya ya Ilala Neema Kiusa, alisema hayo Jimbo la Ukonga kituo cha Afya nguvu Kazi Chanika katika madhumisho ya Siku ya matendo mema Dunia ambayo yameandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo ambapo walishiriki Shughuli za kijamii ikiwemo kupanda miti na shughuli za Usafi .

“Dunia kwa sasa imeharibika viongozi wa dini na Walezi tuwe karibu na watoto wetu tuishi katika misingi Bora ya kumpendezesha Mwenyezi Mungu ikiwemo kufuata mira na Desturi za Kitanzania” alisema Neema .

Mwenyekiti Neema aliwataka wazazi na Walezi wawalehe watoto wao katika misingi Bora Ili watoto wetu waweze kujitambua na kuwataka watoto walindwe wasinyanyaswe Ili kupata Taifa Bora .

Akizungumzia Kampeni ya upandaji miti ambavyo amezindua Jimbo la ukonga iliyoandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo alisema amepongeza Taasisi hiyo kwa kuunga mkono Juhudi za serikali katika sekta ya utunzaji mazingira Fahari Tuamke Maendeleo imekuwa mstari wa mbele.

Suala la kupanda miti ni jukumu letu sote tuishi katika Mazingira Bora ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kila mkoa na WIlaya zipande miti Kila mwaka Ili kulinda Mazingira na vyanzo vya maji “ alisema.

Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau alisema leo ni Siku ya matendo Mema Duniani wameungana na Umoja WANAWAKE WIlaya ya Ilala UWT katika Shughuli za kijamii usafi Usafi pamoja na kupanda miti ya matunda na kivuli .

Neema Mchau alisema ukitenda mema matendo ya ukatili kwa Jamii yatapungua ambapo alitoa wito kwa serikali na Jamii kutenda mema kuondokana na matendo ya ukatili .

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Chanika William Mwilla alisema Wananchi wa Chanika wameungana na Taasisi ya Fahari kwa ajili ya MAADHIMISHO ya Siku ya matendo mema Duniani kwa kuzindua Kampeni ya kupanda miti Jimbo la Ukonga na kufanya usafi kituo cha Afya .

Mwenyekiti Mwilla alisema CCM Chanika ipo na serikali Pamoja katika kusimamia utekelezaji wa Ilani na kazi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Mwisho

Previous articleWANAJESHI KAMBI YA KABOYA KAGERA WAKOSHWA NA WIZARA YA AFYA KUTOA ELIMU KUHUSU UGONJWA WA MARBURG
Next articleDC JOKATE AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUIOMBEA SERIKALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here