Home ENTERTAINMENTS MSAMA: MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAMEKAMIKA, WANANCHI MJITOKEZE KWA WINGI

MSAMA: MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA YAMEKAMIKA, WANANCHI MJITOKEZE KWA WINGI

RAIS wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika April 9 mwaka huu kwenye Viwanja vya Leaders Club Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkuano na waandishi wa habari uliofanyika leo April 1, 2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotion Alex Msama amesema kuwa maandalizi yote ya Tamasha hilo yamekamilika hivyo amewaomba watu wote kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hilo.

“Nataka niwaombe wananchi wa Jiji la Dar es Salaam waje kwa wingi kwenye Tamasha hili , tuungane kwa pamoja kumshukuru Mungu”

“Tamasha la Pasaka halijafanyika kwa takribani miaka tisa hivyo tujitokeze kwa wingi, Tamasha la Pasaka halina kiingilio litafanyika Bure katika viwanja vya Leaders Club” amesema Msama.

Aidha amesema kuwa Jeshi la polisi Mkoa wa Kinodoni wamewakikishia usalama wa kutosha kwa kuimarisha doria viwanjani hapo kwaajili ya usalama wa wananchi wote watakaoudhuria kwenye tamasha hilo.

Previous articleRITA YATAMBULISHA MFUMO MPYA WA KIDIGITALI (eRITA) KWA WAHARIRI
Next articleWAZIRI MKUU AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA 12 WASIMAMIE LISHE BORA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here