Home BUSINESS KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA (PIC) YARIDHISHWA NA KASI UENDELEZWAJI MIRADI...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA (PIC) YARIDHISHWA NA KASI UENDELEZWAJI MIRADI YA NHC

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Slaa (wa nne mwenye shati nyeupe) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah (kulia) alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo wakati Kamati hiyo ilipotembelea Mradi wa Morocco Square Jijini Dar es Salaam, leo Apri 30, 2023.

Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya (PIC) wakiwa na Menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika moja ya maeneo ya Jengo la Morocco Square litakalokuwa na Makazi ya watu, Maduka Makubwa na Hoteli.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Jerry Silaa (katikati), akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Morocco Square samuel Metili (kushoto) wakati Mwenyekiti huyo alipokuwa akikagua vymba katika Makazi yaliyojengwa kwenye Mradi huo. (kulia) ni, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa (NHC) Bw. Muungano Saguya.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Jerry Silaa, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah (katikati) pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika chumba kimojwapo cha hoteli iliyopo katika Mradi huo. Hoteli hiyo ina vyumba zaidi ya 80.

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) Jerry Silaa, akiangalia ujenzi uliofanywa katika Hoteli hiyo.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imefanya ziara kukagua miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika Jiji la Dar es Salaam na kuonesha kuridhika na kasi ya uendelezaji wa Miradi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo iliyofanyika leo April 30.2023, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Slaa, amesema kuwa ni wazi kwamba miradi mingi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ilikuwa imesimama kwa muda mrefu lakini Serikali yaawamu ya Sita ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeliwezesha Shirika hilo kwa kutoa fedha ili kuiendeleza.

Akizungumzia mradi wa Morocco Square ambao sasa umefikia katika hatua za mwisho, amesema licha ya kuwa na makazi ya watu lakini pia kutakuwepo na fursa za ajira kwa watanzania kutokana na uwekezaji mkubwa uliopo katika mradi huo.

“Mradi huu mara utakapoanza rasmi kufanyakazi utatoa fursa za ajira kwa watanzania kwa kuzingatia uwekezaji uliopo kama Hoteli ‘Shopping Mall’ na maeneo mbalimbali ya Biashara” amesema Silaa.

Ameongeza kuwa zira ya kamati hiyo kutembelea na kukagua maendeleo ya miradi hiyo imejionea miradi ambayo ilikuwa inakwama kwama kwa muda mrefu lakini sasa miradi yote imeanza kuendelezwa. “Mradi wa Morocco mmeona Mkandarasi anaendelea na kazi, mradi wa 7/11 unataka kuanza,  na Mradi wa Samia housing Scheme unaendelea kujegwa.

“Tunampongeza Raisi wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuifufua miradi hii, mahitaji ya nyumba Tanzania bado yapo juu sana, lakini Shirika hili ndio mkombozi kwa makazi sababu zipo njia mbili ya kumiliki nyumba,  ya kwanza kutafuta kiwanja chako mwenyewe, kujenga, ama kupitia Shirika la nyumba ambapo utapata nyumba iliyokamilika” ameongeza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah amesema kuwa Shirika hilo limekuwa na utaratibu mzuri wa kujadili mambo mbalimbali  ikiwemo mawazo mazuri kutoka kwenye kamati.

“Kwa niaba ya menejimenti ya Shirika la Nyumba la Taifa, lakini vilevile na Bodi ya Shirika, kwanza nashukuru Kamati ya Bunge kwa kutenga muda wao kwa kuthamini majukumu ambayo wamepewa na Taifa hili ya kusimamia Mashirika ambayo yanafanya Uwekezaji.

“Leo tunajadili kuhusu miradi mitatu kama alivyozungumza na Mwenyekiti, tumezungumzia mradi wa Morocco Square ambao ni Mradi mkubwa wa kipekee Tanzania na Afrika Mashariki, huwezi kukuta mradi mkubwa ambao una shopping Mall, Hotel ya kisasa, Maofisi pamoja na Makazi katika msingi Mmoja.

“Ni jengo la kipekee ambalo lina Quality ya juu ambalo muda si mrefu tutaanza kuwakaribisha wapangaji katika maeneo ya Shopping Mall kuanza kufanya marekebisho kwaajili ya kuanza Biashara. Mradi umekamilika kwa asilimia 100”amesema Abdallah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here