Home LOCAL PAP YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WABUNGE JUU YA USIMAMIZI WA UHAMIAJI...

PAP YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WABUNGE JUU YA USIMAMIZI WA UHAMIAJI BARANI AFRIKA

 

Wabunge kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaowakilisha katika Bunge la Afrika, Mhe. Toufiq Salim Turkey (kushoto, Mhe. Anatropia Theonest na Mhe. Ng’wasi Damas Kamani (kulia) wakiwa kwenye Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) Barani Afrika iliyoandaliwa na Bunge la Afrika.
Bunge la Afrika (Pan – African Parliament – PAP) limeendesha Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika.
Warsha hiyo (Capacity building training workshop on labour migration governance and administration for members of Pan – African Parliament)  inafanyika leo Jumanne Machi 14,2023 na Machi 15,2023 katika Ukumbi wa Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. 
 
Miongoni mwa sababu zilizotajwa kusababisha ongezeko la watu kuhama nchi zao ni pamoja na ukosefu wa Kazi na Ajira kwa vijana  baada ya kuhitimu masomo ya Chuo katika nchi za Afrika hali inayochangia kuhamia maeneo ili kutafuta ajira.
 
Tazama matukio katika picha wakati wa warsha….. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog.
Washiriki wa Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika wakipiga picha ya pamoja.
Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika ikiendelea.
Previous articleMAKAMU WA RAIS WA MAREKANI KUTEMBELEA TANZANIA
Next articleBoT YATOA TAMKO LA KAMATI YA SERA YA FEDHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here