NA TIMA SULTANI
KOCHA Mkuu watimu ya Taifa ya Tanzania ‘ Taifa Stars’ , Adel Amrouche, amewaongeza kwenye kikosi hicho wachezaji wa Simba Mohammed Hussein na Shomari Kapombe .
Timu hiyo inakabiliwa namchezo wa marudiano wakuwania kufuzu kucheza mashindano ya AFCON dhidi ya Uganda unaotarajia kuchezwa Machi 28 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mchezo wao wa kwanza ulichezwa nchini Misri na Stars kuibuka na Ushindi wa bao moja kwa buyu dhidi ya wapinzani wao hao ambao ndio walikuwa wenyeji.
Akiza na Vyombo vya Habari jana, Rais wa Shirikisho la Soka la nchi (TFF) Wallace Karia amesema kulikuwa namaneno mengi lakini mwalimu mwenyewe ndio alichagua hiyo timu na alikuwepo hapo miezi miwili alikuwa akiangalia ligi na hakushtukizwa timu niyeye mwenyewe alichagua baada ya kufuatilia.
“Tunacheza na Uganda ambao katika eneo hili niwashindani wetu tunapocheza Chan na Afcon hii nimara ya pili kukutana nao kwenye AFCON mara ya kwanza tulikufuzu sisi nawao na matokeo hawajawahi kutufunga kwenye mashindano hayo, lakini hilo halitusababishi sisi kubweteka maana wanajipanga kama tunavyojipanga,”alisema
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakubu, amesema Anampongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa mchango wake mkubwa katika michezo pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, hivyo alikabidhi tiketi za kuingilia uwanjani ambazo serikali imezinunua kwaajili yakupatiwa mashabiki.