Home SPORTS MWANA FA KUZINDUA RASMI MASHINDANO YA RAMADHAN CUP JIJINI DAR LEO

MWANA FA KUZINDUA RASMI MASHINDANO YA RAMADHAN CUP JIJINI DAR LEO

NA: TIMA SULTANI

MASHINDANO ya Ramadhan Cup, yanatarajia kuanza kurindima leo kwa mchezo kati ya Silent Ocean na Discount Centre Saa 4:00 Usiku katika viwanja vya JMK Park uliopo Jijini Dar es Salaam.

Timu zitachuana kwenye mashindano hayo zikiwania zawadi nono ambazo zitatolewa na waandaaji wa mashindano hayo Silent Ocean Simba wa Bahari.

Mgeni rasmi kwenye mashindano hayo atakuwa ni Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma (Mwana FA).

Akizungumza na Waandishi wa Habari Machi 26,2023 Jijini Dar es Salaam, Mratibu wa mashindano hayo Iddi Godigodi, amesema Ramadhan Cup ya msimu huu nitofauti na misimu yote ambayo imewahi kupita na kwamba msimu huu utakuwa niwakipekee sana.

Amesema mwezi wa ramadhani ni mwezi wa watu kufanya ibada lakini pia watu kufurahi hivyo vijana wajitokeze kwa wingi kushiriki, lakini pia makampuni ba watu mbalimbali wakutane kubadilishana mawazo.

“Mkurugenzi ameniagiza kwamba michuano hii itakuwa nibora kuliko michuano yote iliyopita kutakuwa na Kipa Bora, Mchezaji Bora, Mfungaji Bora nakadhalika,” amesema.

Amesema kuwa watakaofungua mashindano hayo ni Silent Ocean dhidi ya Wanahabari na mshindi wa mchezo huo ataondoka na Shilingi Milioni tano.

Mmoja wa viongozi wa kampuni ya Silent Ocean ‘Head of Warehouse’ na Mtendaji Mkuu wa mashindano hayo , Amar Burbain, amesema wao kazi yao kubwa ni kusafirisha mizigo kutoka China aambpo huko wapo kwenye miji mitatu ambayo ni Guangzou, Yiwu na Keqiao. Pia wapo Marekani katika Jiji la Washington DC, pamoja na Dubai wakifanyakazi kama Kilimanjaro Star Cargo na Uturuki kama Simba wa Bahari.

Mmoja wa viongozi wa kampuni ya Silent Ocean ‘Head of  Warehouse” na Mtendaji Mkuu wa mashindano hayo , Amar Burbain, amesema wao kazi yao kubwa ni kusafirisha mizigo kutoka China aambpo huko wapo kwenye miji mitatu ambayo ni Guangzou, Yiwu na Keqiao. Pia wapo Marekani katika Jiji la Washington DC, pamoja na Dubai wakifanyakazi kama Kilimanjaro Star Cargo na Uturuki kama Simba wa Bahari.

Previous articleWAZIRI MKUU AAGIZA STENDI KUU BARIADI ITUMIKE KWA MABASI MAKUBWA NA MADOGO
Next articleKAPOMBE, MOHAMED HUSSEIN WAITWA STARS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here