Jengo lililokuwa linatumiwa na Hospital ya Rufaa Ya Mkoa wa Geita kuhifadhia dawa zilizokwisha mda wake limeteketea kwa Moto baada ya moto kuzuka katika jengo hilo huku chanzo cha moto huo mpaka sasa hakijajulikana.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema jengo hilo ni Mali ya Halmashauri ya mji wa Geita na lilikuwa linatumiwa na Hospital teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita kuhifadhia Madawa yaliyokwisha mda wake.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa INSP. Edward Lukuba amesema wamefika eneo la tukio moto ukiwa unawaka na juhudi za Jeshi hilo zimefanikiwa kuudhibiti ili usiathili maeneo mengine jirani.
Amesema moto wameuthibiti ila kuna vyumba viwili ambavyo vilikua na madawa mengi hali inayosababisha moto huo kuendelea kuwaka kwa kasi na wanafanya shughuli ya kuyatoa ili moto huo waweze kuudhibiti.
Nao baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo wamesema wameona moto ukizuka juu ghafra huku wakiwa hawajui chanzo chake hali iliyowafanya kulitaarifu Jeshi la zima moto kwa lengo la kuja kuudhibiti moto huo.
Juhudi bado zinaendelea kwa lengo la kubaini thamani ya vitu vilivyoteketea katika Jengo hilo.