Home LOCAL CoRI WAKETI KUPITIA VIFUNGU VYOTE MUSWADA WA SHERIA YA HABARI JIJINI DAR

CoRI WAKETI KUPITIA VIFUNGU VYOTE MUSWADA WA SHERIA YA HABARI JIJINI DAR

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akizungumza katika mahojiano maalum kuelezea kikao cha Wadau wa haki ya Kupata habari nchini (CoRI) waliokutana hivi karibuni Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupitia vifungu vya muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 baada ya kuwasilishwa Bungni kwa mara ya kwanza mwezi Februari Mwaka huu.

Na: Hughes Dugilo, DSM

WADAU wa Haki ya Kupata Habari nchini (CoRI), wamekutana kwa lengo la kupitia vifungu mbalimbali vya muswada wa mabadiliko ya sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 uliowasilishwa Bungeni kwa mara ya kwanza mwezi Februari mwaka huu.

Wadau hao wamekutana hivi karibuni Jijini Dar es salaam na kupata fursa ya kupitia vifungu vyote 67 viivyopo kwenye Mswada huo ambapo wameipongeza Serikali katika maeneo ambayo wamefanyia maboresho huku wakianisha maeneo ambayo hayajaguswa kabisa.

Akizungumza katika mahojiano maalum siku chache baada ya kikao hicho Jijini humo mmoja ya wajumbe wa Kikao hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amesema wameona Serikli imepitisha  vifungu vinavyoondosha kadhia kwa waandishi wa habari na hivyo kuipongeza Serikali katika maeneo hayo pamoja na maeneo mengine.

“yapo maeneo mengine ambayo wamerekebisha baadhi ya vifungu vikiwa ni pamoja na kuondoa kashfa kuwa jinai na maeneo mengie, mfano Mkurugenzi wa Idara ya Habari alikuwa na mamlaka ya kupanga matangazo sasa yameondoshwa, mitambo ingeweza kukamatwa na Afisa Polisi na kuitaifisha, haya yote yameondoshwa, hivyo tunaishukuru sana Serikali” amesema Balile.

Aidha amefafanua kuwa mwzi 8 mwaka 2022 kulikuwa na Jedwali la mapendekezo ya mabadiliko kutoka upande wa Serikali lakini katika mabadiliko ambayo yamefikishwa Bungeni kuna baadhi ya mambo hayamo huku akibainisha moja ya mambo ambayo walikuwa wakisisitiza ni kifungu cha 9 ambayo matokeo yake yanazaa kifungu cha 10 ambacho kinampa mkurugenzi wa Idara ya habari mamlaka ya kutoa leseni na baadae kuziondosha hizo leseni bila kuwa na utaratibu maalumu wa kushauriana.

“Tumejadili kwa kina  tumebaini kuwa yapo mapendekezo ambayo walikuwa wameyatoa kama Serikali yamebaki vilevile au hayakuingizwa, na tumegundua kwamba tatizo lipo katika sheria na tafsiri ya sheria  ambacho kifungu chake cha 47 kinasema bayana kwamba mtu ambaye ana mamlaka ya kutoa leseni, anakuwa na mamlaka ya kuifuta”

“Vyombo vya habari kama Magazeti, Kampuni inapoanzishwa inapewa leseni na Halmashauri husika inapofanyia Biashara kwa hiyo tunaona hapa kwanza kunakuwa na dhana ya kuwa na leseni mbili kwa Biashara ile ile moja, kwa hiyo tukasema msajili wa magazeti aendelee na kazi ya usajili kwa kuandikisha magazeti alafu magazeti yaendelee kupata leseni kutoka Halmashauri ya Mji” amefafanua.

Akizungumzia ushiriki wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika mchakato mzima wa kuhakikisha Muswada huo unawasilishwa Bungeni amesema kuwa Jukwaa hilo pengine ndio wadau wenye masilahi mapana zaidi kwenye muswada huo kwani inapofikia hatua ya kushitaki gazeti anaeshitakiwa ni Mhariri wa habari pekee na kwamba hata wamiliki wa vyombo husika hawahusishwi.

“Tutaendelea kushikana mikono kuona nchi yetu inapata sheria bora na kuondoka katika unyonge wa kuwa katika zile namba mbaya na kuwa namba moja kwani hata hizo zinazokamata namba moja zinaendeeshwa na Binaadamu”

“Tunaamini kwamaba maslahi ya wanahabari yatapatikana ikiwa sheria imefanyakazi ya kuweka mazingira bora na mazuria,” amesema.

Previous articleHASSAN MWAKINYO KUZICHAPA NA MKONGO KUCHANGIA TAULO ZA KIKE
Next articleJENGO LA KUHIFADHIA DAWA ZILIZOKWISHA MATUMIZI LATEKETEA KWA MOTO GEITA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here