Home SPORTS GRUMETI FUND YAWAKUMBUSHA VIJANA WA KIUME KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA JAMII

GRUMETI FUND YAWAKUMBUSHA VIJANA WA KIUME KUTIMIZA WAJIBU WAO KATIKA JAMII

Kampuni ya Grumeti Fund kupitia Idara ya maendeleo ya Jamii imewakumbusha vijana wa kiume Wilayani Serengeti kutekeleza majukumu yao katika jamii zinazowazunguka.

Akizungumza katika Kongamano la vijana wa kiume lilofanyika tarehe 25 Machi 2023 waliotoka shule za Sekondari Serengeti na Nyichoka Mgeni Rasmi Mwl. Wandere Pamba Rwakatare ambaye ni afisa elimu sekondari wa Bunda Vijijini, amewakumbusha vijana hao kuhakikisha wanatelekeza wajibu yao ipasavyo katika jamiii ikiwemo kuwalinda na kuwapa vipaumbele vijana wa kike sambamba na kujisimamia ili waweze kutimiza ndoto zao.

“Vijana wa kiume tunawajibu wa kutimiza ndoto zetu,Lakini pia tunawajibu wa kuhakikisha kwamba binti unayeishi naye Katika jamii yako naye anatimiza ndoto zake,elimu unayoipata ikusaidie kuionyesha jamii ambayo unaishi nayo kwamba tunazo mila ambazo zinamkandamiza mtoto wa kike ambazo kwa sasa azistahili’’ amesema Mwl.Rwakatare

Mwl. Wandere Pamba Rwakatare aliongeza kwa kusema pia mabinti katika ngazi za elimu ya chini hawafanyi vizuri kutokana na mikandamizo ambayo tunayo katika jamii,lakini mtu ambaye anastahili kumlinda huyo binti ni wewe kaka yake, wewe ni jeshi linalomzunguka binti,uwe askari wake akiwa shuleni ,nyumbani au njiani ili tunapotaka kufikia ndoto zetu tufikie kwa pamoja’’.

Kwa upande wake Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamiii ya Kampuni ya Grumeti Fund Frida Mollel amewasihi Vijana hao kuwasehemu ya mabadiliko chanya katika kutimiza majukumu yao.

‘’Wanaume wana Nguvu kubwa sana katika agenda ya kumuwezesha binti kufikia ndoto zake kuanzia mdogo, wakiwa mashuleni, makazini lakini pamoja na majumbani.Tupige vita mila na desturi zisizo na tija’’

Frida ameongeza pia badala ya mtoto wa kiume na kike kuwa washindani ni vema kuinuana ili kwenda sambamba, amehimiza pia vijana kutojiingiza katika matendo maovu yanayosabishwa na makundi rika na kuiga tabia zinazoletwa na utandawazi.Mkatekeleze yote mliyojifunza kwenye kongamano hili’’Nao vijana walioshiriki katika kongamano hilo wameishukuru Kampuni ya Grumeti Fund kwa kutoa elimu na kuahidi kuwa mabalozi wazuri na kutekeleza yote waliyoelekezwa katika kongamano hilo.

Kongamano hilo lilofanyika katika shule ya sekondari serengeti limewafikia Vijana wa kiume 416 ,ambapo Jezi na mipira kwa timu kutoka shule za sekondari nyichoka na Serengeti zilitolewa, aidha vijana hao walishiriki katika Michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Miguu , kukimbia na yai kwenye Kijiko ,kukimbia kwenye viroba na zawadi kwa washindi kutolewa.

Previous articleTASAC YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA BIASHARA MTWARA
Next articlePROF. NDALICHAKO ATOA RAI KWA WANANCHI WA MTWARA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here