Home Uncategorized SERIKALI YAONGEZA WIGO ELIMU YA JUU

SERIKALI YAONGEZA WIGO ELIMU YA JUU

Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Profesa Charles Kihampa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili ya Uongozi wa Serikali ya awamu ya sita.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria – TCU Benard Kongolo (katikati) pamoja na  Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari Maelezo Zamaradi Kawawa wakifuatilia taarifa ya utekelezaj wa majukumu ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya awamu ya sita Leo Jijini Dodoma.
Na: Janeth Raphael, Michuzi Blog – DODOMA
SERIKALI imeendelea kutekeleza kwa vitendo azima yake ya kuongeza wigo wa fursa za masomo ya elimu ya juu kwa Watanzania katika kipindi cha miaka miwili.
Nafasi za masomo katika vyuo vya elimu ya juu katika program za shahada ya kwanza zimeongezeka kutoka 157,770 mwaka 2020/2021 hadi 172,168 mwaka 2020/2022 ongezeko hilo la nafasi 14,398 ni sawa na asilimia 9.1.
Profesa Charles Kihampa ni Katibu Mtendaji Tume ya vyuo Vikuu Tanzania ameyabainisha hayo leo jijini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari akielezea utekelezaj wa majukumu ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Profesa Kihampa amesema programu za masomo zimeruhusiwa kudahili wanafunzi wa shahada ya kwanza ambapo imeongezeka kutoka 686 mwakae 2020/2021 hadi 757 mwaka 2022/2023, waliodahiliwa katika shahada ya kwanza wameongezeka kutoka 87,934 mwaka 2020/2021 hadi 113,383 mwaka 2022/2023 sawa na asilimia 28.9.
Idadi ya wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu imeongezeka kutoka 259,266 mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2021/2022 sawa na asilimia 14.1 na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kwa mwaka wa masomo aa 2022/2023.
“Kutokana na hatua hizi zinazochukuliwa na Serikalie vyuo Vikuu vimeweza kuimarisha mifumo yake ya uthibiti ubora na uendeshaji wa mafunzo” Profesa Kihampa.
Aidha Profesa Kihampa amesema Tume ya vyuo vikuu Tanzania imeendelea kuandaa na kuratibu mafunzo kwa viongozi, wahadhiri na maofisa wa vyuo vikuu vya umma na binafsi hapa nchini Kwa lengo la kuwajengea uwezo katika usimamizi na uendeshaji wa Taasisi zao.
Hata hivyo Profesa Kihampa amesema kutokana na auelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya TCU na taratibu za uendeshaji wa Elimu ya chuo kikuu kumepunguza kwa kiasi kikibwa changamoto wanazokutana nazo wanafunzi na wadau wengine wa elimu ya juu katika kipindi hiki ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Previous articleWANAFUNZI MBINGA GIRLS WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUJENGA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA
Next articleBIMA YA AFYA KWA WOTE MWAROBAINI WA KUONDOA MADHAIFU YA CHF-DKT MOLLEL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here