Home LOCAL KARIBUNI TUENDELEE KUBORESHA SEKTA YA AFYA NCHINI: WAZIRI UMMY MWALIMU

KARIBUNI TUENDELEE KUBORESHA SEKTA YA AFYA NCHINI: WAZIRI UMMY MWALIMU

 Na: WAF – Dodoma

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewakaribisha Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe na kuwataka kuendeleza ushirikiano ili kuboresha sekta ya Afya nchini.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo katika hafla fupi ya kuwakaribisha makatibu wakuu hao iliyofanyika Ofisi za Wizara Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma.

Waziri Ummy amemkaribisha Dkt. Shekalaghe kwenye menejimenti yake ya kwanza kama Katibu Mkuu na Dkt. Grace Magembe kama Naibu Katibu Mkuu mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Waziri Ummy amewataka Wakurugenzi na watumishi wote kutoa ushirikiano kwa Viongozi hao kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya kama ambavyo Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka.

“Sekta ya afya ni kubwa hivyo tushirikiane kuondoa changamoto ili wananchi wapate huduma zilizo bora na zinazostahili, tuwasimamie wataalamu wetu wa afya hili ni jukumu letu kwa pamoja,” amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalaghe amemshukuru Waziri Ummy kwa ukaribisho mzuri na ameahidi utumishi bora katika nafasi aliyoteuliwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma za afya.

Naye, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano katika maendeleo ya Sekta ya Afya.

Previous articleTANZANIA NA BENKI YA DUNIA YASAINI MKATABA WA MIKOPO NAFUU NA MISAADA YA SHILINGI TRILIONI 1.3
Next articleKINANA AFUNGUA MKUTANO WA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA TANZANIA NA BURUNDI PAMOJA NA KUZUNGUMZA NA KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE LA TANZANIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here