Home LOCAL WAZIRI WA MASUALA YA UCHUMI WA FINLAND AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA...

WAZIRI WA MASUALA YA UCHUMI WA FINLAND AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mhe. Mika Tapani Lintilä amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 29 Januari hadi tarehe 1 Februari 2023.

Lengo la ziara hiyo ni kujadili masuala yenye maslahi kwa Tanzania na Finland ili kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kupitia Programu ya sasa ya Ushirikiano wa Maendeleo na biashara na kukuza ushirikiano wa kibiashara katika sekta ya biashara na uwekezaji.

Mhe. Lintilă akiwa nchini anatarajia kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Pindi Chana, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf F. Mkenda.

Wengine ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC); Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Shirika la Umerne Tanzania (TANESCO).

Previous articleNAIBU WAZIRI MASANJA AHAMASISHA WANANCHI KUPANDA MITI ILI KUTUNZA MAZINGIRA
Next articleDAWASA KUZIMA MTAMBO RUVU CHINI KWA SAA 36
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here