Home LOCAL NAIBU WAZIRI MASANJA AHAMASISHA WANANCHI KUPANDA MITI ILI KUTUNZA MAZINGIRA

NAIBU WAZIRI MASANJA AHAMASISHA WANANCHI KUPANDA MITI ILI KUTUNZA MAZINGIRA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mary Masanja amewahimiza wananchi kuwa wahifadhi wa mazingira kwa kupanda miti ili kuepukana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayoikumba dunia kama ukame, mafuriko n.k.

Ameyasema hayo leo katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi yanayotarajia kufikia kilele chake Februari 5, 2023.

“Nataka niwakumbushe kwamba uhifadhi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu hivyo tuyatunze mazingira ili yaweze kututunza” amesisitiza Mhe. Masanja.

Ameongeza kuwa Ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kila mwananchi ahakikishe anapanda mti na kuutunza ili uweze kukua.

Amesema kufuatia maelekezo hayo ya Mheshimiwa Rais, Wizara ya Maliasili na Utalii imehakikisha inatumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi kupanda miti hususan katika kipindi hiki cha mvua kwenye maeneo mbalimbali ya nchi ili kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani.

Amefafanua kuwa Mheshimiwa Rais Samia amekuwa kinara wa kuhifadhi mazingira na mwongoza njia katika uhifadhi na pia yeyendiye muasisi wa filamu ya The Royal tour iliyopelekea kila mtu sasa anajua masuala ya utalii na uhifadhi.

Mhe. Masanja amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo katika jiji la Mwanza mathalani fedha za ujenzi wa barabara, meli, daraja la kigogo Busisi na miradi mingine ya maendeleo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Masanja ametembelea Shule ya Sekondari Muhandu iliyopo katika Halmashauri ya jiji la Mwanza kwa lengo la kuhamasisha wanafunzi na wananchi wa eneo hilo kuwa na utamaduni wa kupanda miti.

Akiwa katika shule hiyo, Mhe. Masanja amewahimiza wananchi kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi ( CCM).

“CCM ndicho chama kinachoongoza nchi hivyo tukiunge mkono ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa hiyo pia tumuunge mkono Mheshimiwa Rais ili tuweze kufikisha maendeleo ya wananchi pale mlipo” amesema Mhe. Masanja.

Maadhimisho ya Miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi yalihudhuriwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda ambaye alikuwa mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti UWT Taifa, Zainab Shomari pamoja na viongozi wengine wa UWT Taifa na wanachama wa jumuiya hiyo kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Previous articleMWENYEKITI UWT TAIFA CHATANDA AWATAKA VIONGOZI WA UWT KUSIMAMIA VIZURI FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO
Next articleWAZIRI WA MASUALA YA UCHUMI WA FINLAND AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here