Home LOCAL VIONGOZI WA DINI, WADAU WA SEKTA MBALIMBALI WAJENGEWA UELEWA KUHUSU BIMA YA...

VIONGOZI WA DINI, WADAU WA SEKTA MBALIMBALI WAJENGEWA UELEWA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE JIJINI MWANZA 

 Na. WAF – Mwanza

Serikali kupitia Wizara ya Afya imewajengea uelewa kuhusu Bima ya Afya kwa wote viongozi wa makundi ya Wamachinga, Wakulima, Wavuvi, Wachimba Madini, Bodaboda, Mama Lishe na Kamati ya Amani ya Mkoa wa Mwanza ili wakawe Mabalozi wa kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa Wote katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya wakati akifungua kikao kazi cha kutoa Elimu ya Bima ya Afya kwa Wote kwa makundi mbalimbali jijiji Mwanza

“Sasa tunakuja na maboresho ya Bima ya Afya ambayo itakua ni Bima ya Afya kwa Wote, kila mtu kwa hali yake ya kiuchumi aingie kwenye mfumo wa Bima ya Afya hii”. Amesema Prof. Makubi.

Ameeleza kuwa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote ukipitishwa utaongeza wigo wa wananchi wengi kujiunga katika mfumo wa Bima ya Afya kutoka asilimia 15 ya sasa mpaka asilimia zaidi ya 90 na kuendelea ya Watanzania.

“Serikali makini haiwezi kuacha makundi yote haya muhimu wabaki bila kuwa na uhakika wa matibabu ya afya zao.Hivyo lazima kuweka mpango wa Bima ya Afya kwa wote ambapo mtu akiugua kwa hali yoyote ya kifedha aliyonayo aweze kutibiwa kwa haraka na wakati ili aendelee na shughuli zake za utafutaji”Aliongeza Prof. Makubiu

Previous articleWANANCHI KIJIJI CHA MANGA SINGIDA WAWAKATAA VIONGOZI WAO MBELE YA MBUNGE, MKURUGENZI, WATAKA WAONDOKE NAO
Next articleRAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA KAMISHNA DIWANI ATHUMANI MSUYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here