Home BUSINESS RAIS MSTAAFU SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR AIPONGEZA STAMICO KUFIKISHA MIAKA 50.

RAIS MSTAAFU SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR AIPONGEZA STAMICO KUFIKISHA MIAKA 50.

Mheshimiwa Abeid Aman Karume Rais Mstaafu wa Awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amelipongeza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kufikia miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Tamasha la Tisa la Biashara linalofanyika katika viwanja vya Maisara, Zanzibar kuanzia tarehe 30 Desemba hadi 13 Januari 2023.

Akiongea wakati wa sherehe za ufunguzi huo wa Rais Mstaafu Mhe. Karume amezipongeza Taasisi zilizochangia kufanikisha Tamasha hilo ikiwemo STAMICO.

Ameziasa Taasisi hizo na nyingine nchini kuendelea kuwashika mkono waandaji na kuwataka washiriki kutumia tamasha kubadilishana uzoefu na kujifunza ili liweze kuwa na manufaa kwa wananchi.

Wakati wa ufunguzi Mhe. Karume ameelezea kufurahishwa na ufanisi wa tamasha hili na kuwataka waandaaji kufanya tathimini yakinifu ili kuweza kuainisha changamoto zinazojitokeza.

Aidha amewataka waandaji kuanza maandalizi mapema na kushirikisha wadau wengine kutoka nchi nyingine kwa kupitia balozi zetu zilizoko nje ya nchi na balozi za nchi hizo marafiki zilizopo ndani ya nchi yetu.

Ametoa rai ya kuzishirikisha Taasis za Fedha ili ziweze kufungua madirisha ya kifedha yatakayowasaidia wafanya biashara kupata elimu ya jinsi ya kupata mikopo nafuu kwa ajili ya biashara zao.

Aidha ametoa rai ya kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama ili kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji na biashara.

Akiongea baada ya kupokea tunzo ya udhamini kwa upande wa STAMICO Afisa Uhusiano wa Shirika hilo bi.Bibiana Ndumbaro ameishukuru Tantrade kwa kutambua mchango wetu na ushirikiano wa kibiashara uliopo baina ya Taasisi hizo mbili.

Amesema STAMICO imeamua kushiriki katika Tamasha ili kuweza kuitambulisha Bidhaa mpya ya Mkaa Mbadala ya Kupikia wa Rafiki Briquettes kupitia maonesho hayo ili kuhamasisha matumizi sahihi ya mkaa huo.

Amewashukuru wageni wanaokuja kutembelea banda la STAMICO na kujionea na kununua bidhaa hiyo yenye lengo la kuchangia utunzaji wa mazingira.

STAMICO inashiriki katika Tamasha la hili la Tisa la Biashara sambamba na kutangaza na kuunza bidhaa yake mpya ya Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes. Tamasha hili limeanza mwezi Disemba 30, 2022 hadi Januari 13, 2022 linalofanyika katika viwanja wa Maisara Zanzibar.

Previous articleWAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA SEKONDARI YA WASICHANA YA DKT.SAMIA SULUHU HASSAN, RUVUMA
Next articleWAZIRI AWESO AAGIZA KUPANGIWA KAZI NYINGINE MENEJA WA RUWASA WILAYA YA  KILOSA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here