asyabahis.org www.dumanbet.live pinbahiscasino.com www.sekabet.net olabahisgir.com www.maltcasino.net faffbet-giris.com www.asyabahisgo1.com dumanbetyenigiris.com pinbahisgo1.com www.sekabet-giris2.com www.olabahisgo.com www.maltcasino-giris.com www.faffbet.net www.betforward1.org www.betforward.mobi www.1xbet-adres.com www.1xbet4iran.com www.romabet1.com yasbet2.net 1xirani.com www.romabet.top www.3btforward1.com 1xbet https://1xbet-farsi4.com بهترین سایت شرط بندی
Home LOCAL HUDUMA YA KUJIPIMA VVU MAHALA PA KAZI YAANZA.

HUDUMA YA KUJIPIMA VVU MAHALA PA KAZI YAANZA.

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeanzisha huduma ya kujipima VVU mahala pa kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya vipimo vya VVU kwa watumishi makazini hasa wanaume, ambapo hadi kufikia Desemba 2022 watu wapatao 96,231 wamepatiwa huduma ya JIPIME mahala pa kazi..
Hayo yamejiri leo Januari 13, 2023, Jijini Dodoma wakati wakati Naibu  Waziri  wa Afya Dkt. Godwin Mollel akiwasilisha taarifa kuhusu kuhuisha na kujumuisha maswala ya UKIMWI mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya masuala ya UKIMWI.
“Wizara imeanzisha huduma ya kujipima VVU (JIPIME) mahala pa kazi ili kurahisisha upatikanaji wa huduma ya vipimo vya VVU kwa watumishi sehemu za kazi hususani Wanaume. Hadi kufikia Desemba 2022 watu wapatao 96,231 wamepatiwa huduma ya JIPIME mahala pa kazi.” amesema Dkt. Mollel.
Sambamba na hilo amesema, hadi kufikia Desemba 2022 jumla ya vijana balehe 47,705 (Wavulana 20,329 na Wasichana 27,376) walifikiwa katika shule zipatazo 103 kupitia kampeni ya Kipepeo, huku akibainisha kuwa, Kampeni hii inatarajiwa kufanyika mwaka 2023 katika mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Tanga na Geita. 
Ameendelea kusema kuwa, kwa mwaka 2022 Wizara kwa kushirikiana na TACAIDS na Wizara ya Elimu imeweza kutoa mafunzo ya elimu ya jinsia kwa walimu wapatao 5,033 nchini.
Pamoja na hayo, Dkt. Mollel amesema, hadi kufikia Desemba 2022 kuna vituo vitano (5) vya kutolea huduma za afya katika maeneo ya Geita Gold Mine (Geita), North Mara Gold Mine (Mara), Bulyanhulu Gold Mine Limited (Shinyanga), New Luika Gold Mine (Songwe) na Mererani (Manyara).
Amesema, huduma za VVU zinazotolewa katika migodi hiyo ni pamoja na Upimaji wa VVU, huduma za tiba na matunzo ikiwemo utoaji wa ARV, huduma za tohara, huduma za JIPIME, huduma za dawa kinga (PrEP) na magonjwa mengine ya ngono.
Kwa upande wa wakazi wanaokaa maeneo yasiyifikika kwa urahisi hususani visiwani,  amesema, Wizara imekuwa ikitoa huduma za VVU na UKIMWI kwa njia ya huduma mkoba ngazi ya jamii na baadhi ya maeneo kama visiwa hususani Ziwa Vitoria Mkoani Mwanza huduma hii hutolewa kwa kutumia usafiri wa boti maalum (Fikia boat).
Aidha, Dkt. Mollel amesema, Kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2022 jumla ya kondomu 111,934,600 zilisambazwa nchini ili kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI,  huku kati ya hizo, kondomu 2,806,500 zimesambazwa katika Wizara na Taasisi mbalimbali.
Previous articleWAZIRI BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA WA ZANZIBAR AIPA KONGOLE STAMICO KWA KULETA MKAA MBADALA VISIWANI.
Next articleMWENYEKITI WA CCM WILAYA ILALA APOKEA KERO ZA BARABARA MBOVU TABATA 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea HUDUMA YA KUJIPIMA VVU MAHALA PA KAZI YAANZA.