Home BUSINESS BENKI YA CRDB KUSIMAMIA MFUKO WA FAIDA FUND UNAOENDESHWA NA WATUMISHI HOUSING

BENKI YA CRDB KUSIMAMIA MFUKO WA FAIDA FUND UNAOENDESHWA NA WATUMISHI HOUSING


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amezitaka Taasisi zinazohusika na Maendeleo ya vijana, wanawake na makundi maalum kuanza kuyahamasisha makundi hayo kuwekeza kwenye Mfuko wa Faida uliopo chini ya Shirika la Watumishi (Watukishi Housing Investiments), ili asiwepo mtanzania wakuachwa nyuma katika shughuli za uwekezaji na ukuzaji wa mitaji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfuko huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam, Waziri Jenista amesema mfuko huo ni salama kwa uwekezaji kwani tangu uanzishwe hadi sasa umeonesha mafanikio makubwa kwenye sekta ya uwekezaji na uchumi.

Aidha amebainisha kuwa umiliki wa mfuko huo haubagui kufuatia kiwango cha chini cha uwekezaji kuwa ni kuanzia elf 10 hivyo unatoa fursa Kwa mtanzania yoyote kujiunga.

Kwa upande wa Mtunza Amana wa Mfuko wa Faida (Faida Fund) ambaye ni Benki ya CRDB kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji wake, Abdulmajid Nsekela ameeleza kwamba mfuko huo ni wa kipekee, kwani umezingatia sera mahususi ya huduma jumuishi za kifedha zinazomjali mtanzania wa rika zote ikiwa ni pamoja na kuweza kununua vipande kwa shilingi elfu 10 jambo ambalo linaenda sambaba na sera ya benki hiyo ya kumsikiliza mteja.

Amebainisha kuwa Benki ya CRDB inachangia Zaidi ya asilimia 70 ya wateja wote wanaoshiriki katika masoko ya mitaji na dhamana ambapo Soko la Hisa la Dar es Salaam-DSE kupitia tuzo zake inaitabmbua benki hiyo kama kinara wa huduma bora kwenye masoko ya mitaji.

Aidha amefafanua kwamba, Mfuko wa Faida unakuwa mfuko wa saba katika mifuko ya uwezazaji wa pamoja ambayo benki ya crdb inaisimamia na unatoa fursa pekee ya uwekezaji wa muda mfupi kwa watanzania kuweza kukuza mitaji yao kwa faida lakini pia ni faida kwa watumishi housing kukusanya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hata hivyo amesema kuwa benki imejipanga kusimamia mfuko kikamilifu na kuhakikisha maslahi ya wawekezaji yanalindwa kulingana na waraka wa makubaliano kati ya watumishi housing na crdb katika usimamizi wa mfuko huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama (wanne kushoto) akiongoza zoezi la uzinduzi wa Mfuko wa Faida (Faida Fund), uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam, Januari 14, 2023. Pamoja naye ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro (watatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wapili kulia) pamoja na viongozi wengine. Picha zote na Othman Michuzi

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Faida (Faida Fund), uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es salaam, Januari 14, 2023.



LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here