Home BUSINESS MAAFISA HABARI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WATAKIWA KUONGEZA KASI UTANGAZAJI...

MAAFISA HABARI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WATAKIWA KUONGEZA KASI UTANGAZAJI UTALII KUIFUNGUA DAR ES SALAAM KIUTALII

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka Maafisa Habari/ Uhusiano na Mawasiliano wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuongeza kasi ya kutangaza vivutio vya utalii ili kuifungua Dar es Salaam kiutalii.

Hatua hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour.

Mhe. Mary Masanja ameyasema hayo leo mara baada ya kukutana na Maafisa Habari katika kikao kazi kilichofanyika kwenye Ofisi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) jijini Dar es Salaam.

Mhe. Masanja amesema ni lazima kuifungua Dar es Salaam kiutalii kwa kuwa ndio lango kuu la kupokelea wageni kutoka nchi mbalimbali duniani.

ā€œLazima kila mwezi tuwe na tukio la kiutalii jijini Dar es Salaam na tufanye kwa kushirikianaā€.

Aidha, amesema ni jukumu la kila taasisi kuhakikisha inatangaza vivutio vyote bila kubagua taasisi nyingine.

ā€œTaasisi zote za Wizara ya Maliasili na Utalii zinatunza, zinahifadhi na zinaendeleza utalii hivyo tunachotakiwa kufanya ni kumuunga mkono Mheshimiwa Rais ili kile alichokianzisha kilete matokeo chanya.ā€Mhe. Masanja amesisitiza.

Amewataka maafisa hao kutenga bajeti za kutangaza vivutio vya utalii vya maeneo yao ya kazi kupitia vipeperushi na kuviweka katika maeneo yanayotembelewa na wageni.

ā€œVipeperushi vinatakiwa vionekane katika maeneo yote ambayo watalii wanafika hapa jijini Dar es Salaam kama hoteli, viwanja vya ndege na magari yanayobeba abiria ā€œmadereva taxiā€ wanaopokea watalii ili kuvutia watalii wengi zaidi. Vipeperushi hivyo viwe na vivutio vyote vya utalii vya maeneo yote ya taasisi za Wizara ambazo ni TAWA, TANAPA, TFS na MAKUMBUSHO YA TAIFA.

Sambamba na hilo amezitaka taasisi za Wizara hiyo kuitumia fursa ya meli inayoleta watalii nchini kwa kutangaza ujio wake kwa kualika waongoza watalii kushiriki katika kuwapokea na kuwatembeza katika vivutio mbalimbali vilivyoko jijini Dar es Salaam.

Mhe. Masanja amehitimisha kikao hicho kwa kuwataka maafisa hao kuisemea Wizara kwa nguvu moja ili kufikia malengo ya kuongeza idadi ya watalii nchini.

Previous articleRAIS DKT.MWINYI AFUNGUA HOSPITALI YA WILAYA MICHEWENI PEMBA.
Next articleBORESHENI USIMAMIZI WA MIONGOZO NA KUFUFUA KAMATI ZA HUDUMA ZA AFYA – PROF. MAKUBIĀ 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here