Home BUSINESS WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAZIWA NSIMBO

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAZIWA NSIMBO

*Kiwanda hicho kina uwezo wa kusindika wastani wa lita 10,000 kwa saa*

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kiwanda cha kuchakata maziwa cha MSS kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, Mkoani Katavi ambacho kina uwezo wa kusindika wastani wa lita 10,000 kwa saa.

Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda hicho ambacho uwekezaji wake umegharimu shilingi milioni 600, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kila mwenye uwezo awekeze.

Amesema hayo leo {Desemba 13, 2022} wakati akizungumza na wananchi baada ya kuzindua kiwanda hicho ambacho kwa sasa kinazalisha maziwa ya mtindi na maziwa fresh na kinatarajia kuanza uzalishaji wa Samli hivi karibuni.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa rai kwa wafugaji wanaozunguka kiwanda hicho kuuza maziwa kwa mwekezaji huyo ili waweze kujiongezea kipato na kumwezesha mwekezaji huyo kuwa na uhakika wa malighafi ya kutosha.

Previous articleBARRICK REFUTES NORTH MARA HUMAN RIGHTS ALLEGATIONS
Next articleFCC: HATUNA TAARIFA YA MGOGORO WA KIBIASHIARA KATI YA MAKAMPUNI YA NANOVAS NA EXTRABET
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here