Home SPORTS SIMBA SC YAICHAPA KMC 3-1 KIRUMBA

SIMBA SC YAICHAPA KMC 3-1 KIRUMBA

Klabu ya Soka ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imeendeleza ubabe wa ushindi kwa kuichapa timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Simba ilipata bao la kuongoza katika dakika ya 15 ya mchezo huo likipachikwa kambani na John Bocco akiunganisha krosi safi iliyopigwa na Shomari Kaomben goli lililodumu katika kipindi chote cha kwanza.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kuliwinda lango la mwenzake huku kukionekana kufanyiko mabadiliko kwa timu ya KMC na kuifanya timu hiyo kuongeza kasi katika mchezo huo.

Mshambuliaji wa KMC Sadala Mohamed aliipatia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 51 ya kipindi cha pili akiunganisha pasi safi ya Kenieli Mwambungu.

Iliwachukuwa dakika moja tu timu ya Simba kupachika bao la pilli baada ya kufanya msako katika lango la KMC dakika ya 52 ya mchezo huo kwa shuti kali lililopigwa na Augustine Ocrah na kuifanya Simba kuongeza kwa mabao mawili.

Simba waliongeza bao la tatu likifungwa na mlinzi wa kati Inonga Baker katika dakika ya 72 ya mchezo huo akipiga kichwa kuunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Clatus Chama.

kufuatia matokeo hayo timu ya Simba SC inaendelea kushikilia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Ku ya NBC ikiwa na alama 41 ikiwa nymba ya watani wao wa jadi Yaoung Africans yenye alama 47

Previous articleMAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI IBADA YA KRISMAS DODOMA
Next articleKATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATEMBELEA WAGONJWA TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD NA KUTOA ZAWADI ZA SIKUKUU KWA WAGONJWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here