Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI IBADA YA KRISMAS DODOMA

MAKAMU WA RAIS AKISHIRIKI IBADA YA KRISMAS DODOMA

.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango pamoja na mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakishiriki Ibada ya Misa takatifu ya Sikukuu ya Krismasi iliofanyika katika Parokia ya Kristo mfalme iliopo Veyula mkoani Dodoma leo tarehe 25 Desemba 2022.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango akizungumza na waumini wa Parokia ya ya Kristo mfalme iliopo Veyulamkoani Dodoma mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya Misa takatifu ya Sikukuu yaKrismasi leo tarehe 25 Desemba 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.PhilipMpango ametoa wito kwa watanzania kuongeza jitihada katika kuimarisha ulinzi wawatoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyowakumba hivi sasa.
Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo mfalme iliopo Veyula mkoani Dodoma.
Ametoa wito kwa watanzania kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu kwa matendo ya kikatili kwa Watoto na kuacha dhuluma dhidi yao. 
Aidha amewasihi waumini na watanzania kwa ujumla kutimiza mahitaji ya watoto katika kuwatunza ikiwemo kuhakikisha wanapata elimu.
Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya uwepowa mvua zilizoanza kunyeesha hapa nchini katika kuzalisha mazao pamoja na
kupanda miti ili kuhifadhi mazingira.
Amesema ni muhimu suala la upandaji miti kuanza katika ngazi ya familia kwa kupanda miti mitatu kila familia na hivyo kupendezesha nchi na kulinda mazingira.
Katika ibada hiyo, Makamu wa Rais ameambatana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango na ibada imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme iliyopo VeyulaDodoma Padre Saimon Katembo
Previous articleMAGAZETI YA LEO DISEMBA JUMATATU 26,2022
Next articleSIMBA SC YAICHAPA KMC 3-1 KIRUMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here