Home ENTERTAINMENTS SHAWBIT AMEKUJA NA EP YENYE MAUMIVU, UPENDO NA FURAHA

SHAWBIT AMEKUJA NA EP YENYE MAUMIVU, UPENDO NA FURAHA

Mtayarishaji wa muziki mwimbaji na na mwandishi wa nyimbo za Afro beat ama Afro pop Adegboye Segun maarufu kwa jina la Shawbit ameachia EP yake ya kwanza kabisa katika muziki.

Shawbit ameachia EP yake mpya ya kwanza ambayo imepewa jina la King Shaw ambayo ina nyimbo tano ndani yake na katika nyimbo hizo wimbo ambao unabeba album unaitwa Lamba Limbo, Hello, My Yard, Oje, To my fans.
 
Katika EP hii Shawbit amelenga zaidi maisha ,maumivu, upendo pamoja na furaha katika mambo mbalimbali huku ikiwa imesimamiwa kwa uzuri na Dexter pamoja na Lawd katika upande wa ubunifu na utayarishaji.
 
Unaweza kumpata msanii huyu katika mitandao yake ya kijamii kama @officialshawbit

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here