Wekundu wa Msimbazi SIMBA SC ime fumua timu ya Prisons ya Mbeya jumla ya mabao 7-1 katika mchezo wa Ligi Kuu soka ya NBC Tanzania Bara.
Katika Mchezo huo uliopigwa leo Disemba 30, 2022 katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam timu ya Simba ndio ilikuwa ya kwanza kuliona lango la Prisons goli likifungwa na John Bocco katika dakika ya 12 ya mchezo huo.
Dakika ya 29 ya mchezo huo Prisons walifanikiwa kurudisha goli hilo likifungwa na Jeremiah Juma ambalo lililodumu katika kipindi chote cha kwanza cha mchezo huo.
kipindi cha pili Simba SC ilikuja kwa kasi zaidi na kuanza kuhesabu kalamu ya magoli ambapo dakika ya 45 tu ya kipindi cha pili John Bocco tena aliipatia timu yake bao la pili.
Saido Ntibazonzinza aliipatia timu ya Simba bao la tatu katika dakika ya 60 ya mchezo huo akipokea pasi kutoka kwa Clatus Chama.
Ilichukua dakika tatu ya mchezo huo Saido Ntibazonzinza tena kupachika bao la nne katika dakika ya 63 ya mchezo huo akipokea pasi kutoka kwa Mzamilu yasini.Â
Simba SC ilipata bao lake la tano kwenye mchezo huo likifungwa na John Bocco kwa mpira wa kichwa akiunganisha krosi safi iliyopigwa na mlinzi wa kushoto wa timu hiyo Gadiel Michael ambapo goli la sita lilifungwa tena na Saido Ntibazonzinza katika dakika ya 70 ya mchezo huo.
Shomari Kapombe alishindilia msumari wa mwisho dakika za lala salama ya mchezo huo na kuifanya Simba kuhesabu jumla ya magoli Saba lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo.
Kufuatia ushindi huo Simba SC imeendelea kubaki katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ikiwa na alama 44 nyuma ya Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Young African’s yenye alama 47.