Home ENTERTAINMENTS RUNWAY BAY YATIKISHA ZANZIBAR

RUNWAY BAY YATIKISHA ZANZIBAR

NA: MWANDISHI WETU

KILELE cha tamasha la mitindo Zanzibar Internation Fashion, kikefanyika juzi katika viwanja vya Forodhani kisiwani Unguja kwa wabunifu 12 kuonyesha kazi zao.

Huu ni msimu wa tatu tokea kuanzishwa kwa jukwaa hili ambalo limekuwa likifanyika kila ifikapo mwezi Desemba na kutoa frusa kwa wanamitindo na wabunifu.

Akizungumza na wandishi wa habari muasisi wa jukwaa hilo Waiz Shelukindo, amesema dhima kubwa ya jukwaa hilo ni kutoa frusa kwa wadau wa mitindo na kutangaza utalii wa Zanzibari.

“Kwa kipindi cha miaka mitatu tumefanya jukwaa hili ambalo malengo yetu tumeanza kuyafikia kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wapo wabunifu ambao wamepat frusa nyingi kupitia jukwaa hili na kutanua wigo wa biashara zao kufikia nchi za nje,” alisema Waizi.

Aliongeza kuwa msimu huu walipata bahati ya kutembelea sehemu za utalii pamoja na kufika katika visiwa vidogo vilivyopo ndani ya Unguja na kupiga picha ambazo zitatangaza utalii wa ndani.

Aidha mmoja wabunifu Mtu Moko ambaye naye alionyesha mavazi yake amesena jukwaa hilo limetoa dira kubwa katika maisha yake na kumfanya aweze kujiajiri.

“Niliasha kushiriki katika jukwaa hili kama mwanamitindo ambaye nilikuwa naonysha nguo za wabunifu nilipo maliza tu nikapata mfadhili ambaye alitaka nianze kutengeneza mavazi yangu na huu ni mwaka wa pili tokea niwe mbunifu wa mavazi ambaye nimezaliwa na tamasha hili.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here