Home BUSINESS NAIBU WAZIRI MASANJA ASHAURI WaKANDARASI WENYE MISAMAHA YA KODI ZIJUMLISHWE NA KODI...

NAIBU WAZIRI MASANJA ASHAURI WaKANDARASI WENYE MISAMAHA YA KODI ZIJUMLISHWE NA KODI NYINGINEZO KURAHISISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) amekishauri kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa kwamba Mkandarasi anapopata msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani ( VAT) ijumuishe na kodi nyingine zilizo chini ya Halmashauri ili kurahisisha utekelezaji wa miradi.

Ameyasema hayo leo katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo.

“Ni maamuzi ya busara tukiamua kufanya maazimio ya kuhakikisha tunakamilisha miradi kwa wakati kwa kuweka utaratibu maalum ambao Halmashauri zitapewa taarifa” Mhe. Masanja amefafanua.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Mwanzana Wakuu wa Taasisi mbalimbali Mkoani Mwanza.

Previous articleASHINDWA KUWEKEZA KUTOKANA NA MGOGORO YA ARDHI MLIMBA
Next articleRUNWAY BAY YATIKISHA ZANZIBAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here