Home Uncategorized NAIBU WAZIRI WA FEDHA ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI KUENDELEA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO...

NAIBU WAZIRI WA FEDHA ATOA WITO KWA WAWEKEZAJI KUENDELEA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO TANZANIA

DAR ES SALAAM.

Naibu waziri wa Fedha na Mipango Hamad Hassan Chande amewasihi wawekezaji hapa nchini kuendelea kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ikiwemo za kibiashara na utalii sambamba na kutanua wigo wa biasahara zao ndani ya nchi, Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.

Mhe. Chande ametoa wito huo Jijini Dar es Salaam katika hafla maalum ya Umoja wa Maafisa Watendaji Wakuu wa Makampuni Binafsi nchini (CEOs roundtable) ikiwa na lengo la kujadili maendeleo ya sekta binafsi katika bara la Africa. 

Ameeleza kuwa Sekta Binafsi ina mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa lolote na kwamba Serikali inatambua na kuthamini mchango wao katika nyanja mbalimbali ikiwemo uwekezaji.

Hata hivyo Mhe. Chande amesema kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Sekta Binafsi ili kukuza sekta ya uchumi, kutatau tatizo la ajira na kuongeza ustawi wa maendeleo ya nchi.

Katika hatua nyngine Naibu waziri huyo amewataka wadau wa Sekta Binafsi nchini kutumia mifumo maalumu ya utoaji malalamiko na mapendekezo kwa Serikali juu ya sera na sheria za uwekezaji badala ya kutumia njia nyingine zisizo rasmi kutoa kero zao ikiwemo mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Watendaji wakuu (CEOrt) David Tarimo amesema sambamba na maboresho ya sheria za uwekezaji yanayofanywa na Serikali CEOrt itahakikisha uwekezaji unaendelea kufanyika kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.

Previous article MWENYEKITI WA CCM TAIFA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NDG. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA MKUTANO KUU WA 10 WA CCM KATIKA UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE JIJINI DODOMA
Next articleCHUO CHA BAHARI (DMI) CHAOMBA MIUNDOMBINU YAKE IKARABATIWE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here