Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) amekishauri kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa kwamba Mkandarasi anapopata msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani ( VAT) ijumuishe na kodi nyingine zilizo chini ya Halmashauri ili kurahisisha utekelezaji wa miradi.
Ameyasema hayo leo katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo.
“Ni maamuzi ya busara tukiamua kufanya maazimio ya kuhakikisha tunakamilisha miradi kwa wakati kwa kuweka utaratibu maalum ambao Halmashauri zitapewa taarifa” Mhe. Masanja amefafanua.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Mwanzana Wakuu wa Taasisi mbalimbali Mkoani Mwanza.