Home BUSINESS MHE.MASANJA: MAENDELEO SEKTA YA UTALII YAENDANE NA HUDUMA BORA

MHE.MASANJA: MAENDELEO SEKTA YA UTALII YAENDANE NA HUDUMA BORA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Marry Masanja akizungumza alipohutubia kwenye mahafari ya 20 ya Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) yaliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi Chuo cha taifa cha Utalii Iman Kajura akizungumza alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza.

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na shughuli za Kitaaluma wa Chuo cha taifa cha Utalii (NCT)  Jesca William (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chuo hicho, Bw. Munguabela Kakulima (kulia) katika maandamano ya kitaaluma kuelekea ukumbi wa JNCC kwaajili ya mahafali ya 20 ya chuo hicho yaliyofanyika leo Disemba 2,2022.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Marry Masanja (kulia) pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha taifa cha Utalii (NCT) katika katika maandamano ya kitaaluma wakati wa mahafali ya 20 ya Chuo hicho.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja, ameziagiza taasisi zote za Wizara kutenga nafasi za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kila mwaka ili kuendana na kasi ya ongezeko la wanafunzi na kuchangia upatikanaji wa maeneo ya mafunzo kwa vitendo sambamba na kutoa ajira kwa wanafunzi hao pale nafasi zinapopatikana.

Naibu Waziri Masanja ameyasema hayo leo Disemba 2,2022 katika mahafali ya ya 20 ya Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNCC) Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa maendeleo ya utalii kitaifa yataweza kufikiwa endapo wadau wote watashiriki katika jitihada za kuelimisha, kuendeleza, kukuza na kuitangaza Tanzania na kwamba kwa kuboresha huduma bora kwa utalii kutaongeza tija katika sekta hiyo.

“Hatuna budi kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za utalii zinazotolewa zinabeba weledi unaostahili”

Weledi huu utaonekana vizuri zaidi katika huduma zetu endapo tutaajiri wataalam wenye ujuzi stahiki kama wanaohitimu leo hii.

Ifike mahali nchi yetu tujivunie kutoa wataalam wanaotosheleza soko la ndani na kupata fursa ya kutoa huduma katika soko la nje kama ilivyo kwa jirani zetu.” amesema Mhe.Masanja.

Aidha ametoa rai kwa wadau wa sekta ya utalii chini kuhakikisha kuwa huduma mbalimbali za utalii zinazotolewa zinabeba weledi unaostahili na kwamba hilo litaonekana vizuri zaidi kwa vitendo endapo wataajiri wataalam wenye ujuzi stahiki kama wanaohitimu katika chuo hicho.

“Ifike mahali nchi yetu tujivunie kutoa wataalam wanaotosheleza soko la ndani na kupata fursa ya kutoa huduma katika soko la nje kama ilivyo kwa jirani zetu” amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utalii (NCT) Dkt. Florian Mtey, amesema Chuo hicho kinakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa wataalamu hasa katika fani ya ukarimu na uratibu wa matukio, miundombinu na vifaa chakavu kwa Kampasi ya Arusha na Temeke ambapo inapelekea kuwepo kwa matengenezo ya mara kwa mara pamoja na ukosefu wa mabweni kwaajili ya wanafunzi katika kampasi ya Arusha, Mwanza na Bustani

Aidha amesema pamoja na changamoto zilizopo bado Chuo hicho kimeendelea na majukumu yake kupitia mikakati mbalimbali ikiwemo uanzishwaji wa kampuni inayomilikiwa na Chuo hicho kwaajili ya kuongeza wigo wa biashara mbalimbali ndani na nje ya maeneo ya kampasi.

Aidha Dkt. Mtey amewataka wahitimu hao kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo iliyopo ya utumishi wa umma wakatapokuwa wakitimiza majukumu yao wakiwa kazini.

Katika hatua nyingine Dkt. Mtey amemshukuru Rais wa Jamhurin ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya maliasili na utalii kwa kutoa fedha za mradi wa UVIKO-19 zilizopelekea chuo hicho kutoa mafunzo kwa washiriki 1050 katika mikoa 8 ya Tanzania bara, pamoja na wakaguzi kwa kutambua ubora wa hoteli zilizopo nchini ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma katika sekta ya utalii na hivyo kufikia lengo la serikali na wizara la kuongoza watalii 5000 kufikia mwaka 2025.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here