Home LOCAL KAMPENI YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI YA MGODI WA BARRICK BULYANHULU YAWAFIKIA...

KAMPENI YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI YA MGODI WA BARRICK BULYANHULU YAWAFIKIA WANAFUNZI

Mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga umeungana na Serikali na wadau wengine kuadhimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo umeandaa kampeni ya kutoa elimu dhidi ya vitendo hivyo katika shule za msingi na sekondari zilizopo katika vitongoji vilivyopo jirani na mgodi huo.
 
Kupitia kampeni hiyo wanafunzi walipata fursa ya kufundisha jinsi ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia sambamba na kuuliza maswali kutoka kwa wataalamu wa ustawi wa jamii na jinsia waliokuwa wakiendesha maswali hayo,pia waligawiwa vipeperushi na t-shirt zenye jumbe za kukabiliana na vitendo hivi ambavyo vimekithiri katika jamii.
 
Akiongea kwa niaba ya Wananchi kuhusu maadhimisho haya Afisa Mtendaji wa kata ya Bulyanhulu, Abdallah kombo,alishukuru Barrick Bulyanhulu kwa kufanikisha kampeni hizi ambazo kwa kiasi kikubwa zimeweza kuwajengea uwezo wanafunzi kuelewa jinsi ya kujikinga na vitendo hivyo.
 
Bi. Anna Boniphase mwakalinga Afisa Maendeleo ya Jamii kata Bulyanhulu akiongea na wanafunzi jinsi ya kujikinga na ukatili wa kijinsia
Picha ya pamoja ya walimu,wanafunzi,wakufunzi na wafanyakazi wa Barrick wakati wa kampeni hiyo
Wanafunzi wa shule za sekondari Bugalama na Bulyanhulu wakifuatilia mafunzo ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Mgodi wa Bulyanhulu

Previous articleRAIS DKT. SAMIA AHUTUBIA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI
Next articleCHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) KUFANYA MAHAFALI YA 20 JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here