Home LOCAL AFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAJI AKINAWA MIGUU GEITA

AFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAJI AKINAWA MIGUU GEITA

Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Benjamin John (30) mkazi wa Mtaa wa Nyampa kata ya kasamwa halmashauri ya mji wa Geita, mkoani Geita amefariki dunia kwa kusombwa na maji katika mto Nyampa uliopo Mtaa wa Nyampa kata ya kasamwa Mkoani humo wakati alipokuwa ananawa miguu baada ya kumaliza kulima.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita INSP. Edward Lukuba amesema Mtu huyo amefariki dunia kutokana na ajari ya mafuliko baada ya kumaliza shughuli zake za kilimo kisha kwenda kuoga kwenye mto huo hali iliyosababisha kusombwa na maji.

Mganga mfawidhi wa kituo cha afya kasamwa Emmanueli Alex amethibitisha kutokea kwa kifo hicho amesema mwili wa marehemu ulifikishwa katika kituo hicho na asikari wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Geita na walipoufanyia uchunguzi walibaini amekufa kwa maji na haukuwa na jeraha lolote.

Wananchi wa mtaa wa Nyampa kata ya Kasamwa halmashauri ya mji Geita wameiomba serikali kuwajengea kivuko katika mto huo kutokana na kuwepo na matukio ya mara kwa mara ya watu kuuwawa kwa kusombwa na maji wakivuka kwenda kwenye shughuli zao za kilimo.

Previous articleGENERALI WAITARA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI UWANJA WA GOFU HIFADHI YA SERENGETI
Next articleRAIS WA ZANZIBAR MHE. DKT. HUSSEIN MWINYI AHUTUBIA MAADHIMISHO SIKU YA KILELE CHA MWEZI WA SHUKRANI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here