Home LOCAL WAZIRI MKUU ASHUHUDIA HALI YA UOKOAJI NA KUWAONA MAJERUHI WA AJALI...

WAZIRI MKUU ASHUHUDIA HALI YA UOKOAJI NA KUWAONA MAJERUHI WA AJALI YA NDEGE YA PRECISION BUKOBA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumapili Novemba 6, 2022 amewasili Mkoani Kagera kushuhudia zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia Ndege ya Precision Air kupata ajali ilipokuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewajulia hali wahanga wa ajali hiyo wanaopata matibabu katika hospitali ya mkoa wa kagera.

Akizngumza katika eneo hilo, Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatoa pole kwa wote walioguswa na ajali hilo na kwamba Serikali itaendelea kutoa huduma stahiki kwa majeruhi wote.

Pia, amewataka wananchi wawe na subira katika kipindi hiki ambacho Serikali itafanya uchunguzi kupitia vyombo vyake ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Previous articleMAJALIWA ASHIRIKI IBADA YA KUSIMIKWA ASKOFU
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 7-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here