Home BUSINESS UJUMBE WA ARIPO WAKUTANA NA WADAU

UJUMBE WA ARIPO WAKUTANA NA WADAU

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika ya Miliki Ubunifu la Kanda ya Afrika (ARIPO) Bw. Bemaya Twebaze akizungumza katika Kikao na wadau wa sekta za umma zinazojihusisha na masuala ya ubunifu wa aina mpya za mbegu za mimea (protection of new varieties of plants) kilichofanyika Leo Novemba 1,2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu (BOT) Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Sheria na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Shirika ya Miliki Ubunifu la Kanda ya Afrika (ARIPO) Bw. Pierre Runiga akiwasilisha mada juu ya majukumu ya Taasisi hiyo kwa wadau kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini walioshiriki mkutano juu ya ulindaji wa mbegu mpya za mimea, baada ya majadiliano yaliyofayika jijini Dar es Salaam Agosti 22, 2022. Mkutano huu wa kuwajengea uelewa wadau umefanyika leo tarehe 01 Novemba, 2022 jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi Mchambuzi kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO) Bw. Said Ramadhani akiwasilisha mada juu ya Ulindaji wa Mbegu Mpya za Mimea kwa wadau kutoka taasisi mbalimbali baada ya majadiliano yaliyofayika jijini Dar es Salaam Agosti 22, 2022. Mkutano huu unaofanyika leo tarehe 01 Novemba, 2022 jijini Dar es Salaam una lengo la kuwajengea uelewa wadau.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika ya Miliki Ubunifu la Kanda ya Afrika (ARIPO) Bw. Bemanya Twebaze (aliyeketi katikati), akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau walioshiriki mkutano juu ya ulindaji wa mbegu mpya za mimea baada ya majadiliano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 22, 2022. Mkutano huu wa kuwajengea uelewa wadau umefanyika leo tarehe 01 Novemba, 2022 Dar es Salaam.

Ujumbe kutoka Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), unafanya ziara nchini kwa kukutana na wadau wa sekta za umma zinazojihusisha na masuala ya ubunifu wa aina mpya za mbegu za mimea (protection of new varieties of plants) chini ya Itifaki ya Arusha ya Ulinzi wa Aina mpya za Mbegu.

Ujumbe huo ukiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa ARIPO kutoka Makao makuu nchini Zimbabwe Bw. Bemanya Twebaze umepokelewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), mwenyeji wa ujumbe huo, ambapo kwa kushirikiana na Wataalam hao, umefanya semina kuhusu Itifaki ya Arusha ya Ulinzi wa Aina Mpya za mbegu iliyofanyika Leo Novemba 1, 2022 Jijini Dar es salaam, ili kujadili kwa kina kuhusu ulinzi wa aina mpya za mimea.

Akitoa neno la ufunguzi katika kikao hicho Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa amesema, Tanzania kama mwanachama wa ARIPO, imechukua jukumu hili ili kutoa nafasi kwa wabunifu mbalimbali kupata ufahamu utakaowasaidia kuendelea kulinda haki zao kupitia ubunifu wa aina mpya za mbegu za mimea, ikizingatiwa kwamba mbegu bora zaidi zinahitajika kwa wingi ili kuongeza uzalishaji na kuleta kuhakika wa chakula.

Bw. Nyaisa ameeleza zaidi kwamba “BRELA kama taasisi inayohusika na masuala ya usajili na uhifadhi wa kumbukumbu za bunifu mbalimbali, kwa kuzingatia majadiliano kuhusu ulinzi wa aina mpya za mimea, imetenga fedha katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 ili kuhakikisha wabunifu wanapewa elimu ikiwemo kuwatembelea katika maeneo ya ubunifu na hasa katika vyuo mbalimbali vinavyotoa elimu na kufanya tafiti ili kulinda bunifu zao na kupata faida zitokanazo na ulinzi wa bunifu.

Aidha, BRELA itahakikisha kuwa elimu ya Miliki Ubunifu inawafikia wadau wote wanaohusika ikiwemo ulinzi wa aina mpya za mimea kwa kuandaa semina mbalimbali na mafunzo yenye tija, ili wabunifu wafahamu nini wanachotakiwa kusajili na manufaa ya kuongeza thamani ya bunifu zao”,

Tangu Mwaka 2018 BRELA ilianzisha mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS), ambao umewezesha Usajili kuanzia hatua za maombi mpaka kukamilika na pia mfumo umewezesha wadau kupata taarifa mbalimbali za Usajili wa bunifu.

Kwa upande wake Bw. Twebaze ameshukuru mapokezi mazuri na ushirikiano walioupata kutoka BRELA na kueleza kuwa hali hii itawezesha dhima kuu ya ARIPO ya kuwafikia wadau ambao ndiyo wamiliki wa bunifu hizo na kupata manufaa zaidi.

Bw. Twebaze ameongeza kuwa ujumbe huo umeshatembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na kushuhudia bunifu mbalimbali ambazo zinatia matumaini kuwa uelewa wa masuala ya miliki ubunifu unaongezeka zaidi hivyo Shirika la ARIPO litaendelea kutoa ushirikiano kwa BRELA ili wabunifu wengi zaidi waweze kulinda bunifu zao ikiwemo aina mpya za mbegu za mimea.

Aidha, amewataka wadau waliofika katika semina hiyo kuwa na mchango chanya kwani maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaenda sambamba na ubunifu, hivyo taasisi zinazohusika hazina budi kuungana na kutoa elimu ili wabunifu wengi waweze kulinda bunifu zao.

“Ikiwa kilimo kinazidi kukua kila siku, ulinzi wa aina mpya za mbegu mimea umelenga kuongeza chachu katika ubunifu mpya wa mbegu za mimea na kulinda bunifu hizo na kutambulika katika maeneo mengine”, amesisitiza Bw. Twebaze..

Previous articleMTENDAJI MKUU BRELA ATETA NA MKURUGENZI WA MILKI BUNIFU AFRIKA (ARIPO) JIJINI DAR
Next articleTIMU YA WACHEZA GOLF 12 KWENDA MALAWI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here